Refarii mtajika Howard Webb ameestaafu.
Webb ambaye amepuliza kipenga kwa muda wa miaka 25 amestaafu
baada ya kuchaguliwa kuwa afisa wa shirikisho la marefarii (Professional Game
Match Officials Limited PGMOL).
Kabla ya kustaafu Webb alikuwa muamuzi katika
mechi 500 za
ligi ya Premia ya Uingereza mbali na zile za kuwania ubingwa wa FA.
Hata hivyo kilele cha tajriba yake ilikuwa fainali ya kombe
la dunia la mwaka wa 2010 iliyoandaliwa huko Afrika Kusini .
Refarii huyo mwenye umri wa miaka 43 alianza kazi hiyo mwaka
wa 1989.
"najivunia tajriba niliyonayo na sasa nawashukuru
wenzangu kwa kunichagua kuwahudumia katika kazi hii mpya ," alisema Webb
Refarii mtajika Howard Webb ameestaafu.
Webb amewahi kuamua fainali ya kombe la mabingwa barani
Ulaya fainali ya ligi kuu ya premia ya Uingereza.
Katika kombe la dunia lililokamilika majuzi huko Brazil,
Webb alimua mechi ya kundi Cha baina ya Colombia na Ivory Coast,na ile ya mchujo
baina ya Brazil na Chile.
Amewahi tuzwa na malkia wa Uingereza mwaka wa 2011na tuzo la
MBE .
No comments:
Post a Comment