Inasemekana kuwa huyu mtoto ameuliwa na baba yake mzazi kwa
kipigo kikali...maeneo ya Moshi Vijijini- kijiji cha Mero...Yaani ukiangalia
Hata picha zake zinaonyesha kabisa jinsi mwili wa huyu mtoto Malaika ulivyojaa
makovu ambayo ni ya kipigo cha mara kwa mara.....Yesu turehemu...
Inasemekana mtoto anakaa na baba yake mzazi na mama wa
kambo... Ebu angalia jinsi huyu mtoto alivyoumizwa jamani..... yaani nimelia
kwa uchungu maana huyu mtoto ameteseka sana kufa
kwake.....alitamani mtu aje
amkamate baba yake ili asiendelee kumpiga lakini hakutokea....alilia sana ili
baba amuache lakini bado akaendelea kupigwa sana.... aliona jinsi baba
anavyomuonea kwa kuwa yeye sii mkubwa kama baba yake hata ajitetee kwa kumzuia
(mfano watu wazima wanavyopambana)
Mwili wa mtoto umeviria damu kwa kipigo toka kwa baba yake
mzazi ambae nimeambiwa anaitwa Morsi Clemence, na mara nyingi shughuli zake ni
vibarua vya hapa na pale...... Natamani sana kufanya kampeni maalumu ya ''OKOA
MTOTO'' ili jamii iwalinde watoto wetu...
Tukio hili limetokea eneo linaloitwa kitu kama kwa ''Raria''
ambapo ni katikati ya njia panda na kabla hujafika Moshi mjini.... jamani huyu
baba naskia amekimbia baada ya kujikuta ameua mwanae kwa kipigo kizito...
Marehemu kazikwa jana baada ya babu mtoto kusema azikwe wakati baba mtoto
(mtuhumiwa) akitafutwa popote alipo....
Mbaya zaidi nimeambiwa kwamba huyu baba ana mke ambae ni
mama wa kambo na huyu mtoto ambae ndiye aliyekamatwa baada ya mume wake
kukimbia kusikojulikana.... BINAFSI NINA MASWALI MENGI BAADA YA KUSIKIA KUNA
MAMA AMBAE ANAISHI NA HUYU BABA ALIYEUA.... MBONA MTOTO ANA MAKOVU MENGI KIASI
HIKI??? KWANI HUYO MAMA HAKUWA ANAMTETEA HUYU MTOTO WAKATI ANAPIGWA NA
BABAKE???? IMENIUMA SANA SANA LAKINI NDO HIVYO..... RIP MY LOVE Naomba kama upo
maeneo haya tuwasiliane 255783137777.CHANZO Wanawake Live
No comments:
Post a Comment