Sunderland imemsajili kiungo wa Manchester City Jack Rodwell
kwa mkataba wa miaka miatno ikiwa ni sehemu ya kukiimarisha kikosi hicho kwa
ajili msimu ujao wa ligi.
Kinda huyo wa
kimataifa wa England, 23, amejiunga na klabu hiyo kwa ada ya paundi 10m.
"Soka la uhakika
ni kitu muhimu sana kwangu," Rodwell aliiambia website ya Sunderland.
"Hii ni sehemu kubwa kwangu."
Rodwell alijiunga na City akitokea Everton kwa ada ya paundi 12m mwaka
2012 lakini amecheza mara 26 tu na kufunga mabao mawili kutokana na kukumbwa na
majeruhi ya mara kwa mara jambo ambalo lilitoa nafasi kwa viungo wengine
kufanya kazi.
Aliichezea Everton kwa mara ya kwanza dhidi ya AZ Alkmaar
December 2007, akiwa na umri wa miaka 16 na siku 284 - na kuwa mchezaji mdogo
zaidi kuiwakilisha Everton Europe
Alicheza michezo 85 akiwa na the Toffees, na kufunga mara
nne
Alijiunga na Manchester City kwa uhamisho wa paundi 12m na
kusaini mkataba wa miaka mitano August 2012
Alicheza micheo 16 na kufunga mara mbili akiwa na City
Aliichezea England
kwa mara ya kwanza katika mchezo dhidi ya Uhispania ambapo walishinda 1-0
November 2011 na akaichezea katika michezo dhidi ya Sweden na Brazil
No comments:
Post a Comment