Pages

Tuesday, August 19, 2014

JOSE MOURINHO AMPOZA KIAINA PETR CECH BAADA YA KUMBWAGA BENCH

JOSE Mourinho amesisitiza kuwa anahitaji kumbakisha kipa wake Petr Cech katika klabu ya Chelsea, licha ya kumuanzisha Thibaut Courtois kwenye mechi ya ufunguzi wa ligi kuu England jana usiku dhidi ya Burnley ambapo alishinda kwa mabao 3-0.Cech amekuwa akihusishwa kujiunga na klabu mbalimbali zikiwemo PSG na Real Madrid, kufuatia kurejea kwa Courtois aliyecheza kwa mkopo kwa misimu mitatu katika klabu ya Atletico Madrid.


 Lakini inafahamika kuwa Chelsea wapo tayari kusikiliza ofa nzuri juu ya kipa huyo mwenye miaka 32.
 “Naamini hakuna mtu atakayekuja na naamini ninachokisema, naweza kuwa na makipa bora watatu na itakuwa nzuri sana,” aliwaambia Sky Sports.
 “Lakini heshima ya kwanza ni kumbakisha klabuni kwasababu tunahitaji makipa wa kiwango cha juu, jumlisha Mark (Schwarzer) ambaye ni kipa mkubwa”

No comments:

Post a Comment