Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohd Shein akiifungua rasmi michezo ya Majeshi ya Afrika Mashariki, kwenye Uwanja wa Amani mjini zanzibar leo.
Kikundi cha Utamaduni cha Jeshi la Kujenga Uchumi Zanzibar { JKU } Kitoa burdani wakati wa ufunguzi wa michezo ya majeshi ya Afrika ya Mashariki kwenye uwanja wa amani mjini Zanzibar.
Vijana wa jeshi la Rwanda wakifanya vitu vyao walipocheza ngoma ya asili ya nchi hiyo kwenye ufunguzi wa michezo ya Majeshi ya Afrika ya Mashariki amani Mjini Zanzibar.
Vijana wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania { JWTZ } wakirusha njiwa hewani kama ishara ya ufunguzi baada ya kumalizika kwa Hotuba ya ufunguzi wa mashindano ya michezo ya majeshi ya afrika mashariki.
Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na Timu ya Soka ya Burundi kabla ya kuanza kwa pambano lake dhidi ya Tanzania mara baada ya kuzindua rasmi michezo ya majeshi ya afrika ya Mashariki kwa niaba ya Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohd Shein.
Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Majeshi, waamuzi na wadhamini wa michuano hiyo. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
Alisema michezo hii hutoa msisimko katika kipindi chote cha mashindano na kuacha matokeo mazuri kwa wananchi katika kuipenda jambo ambalo hufufua ari ya kuiendeleza michezo kwa nchi mwenyeji kwa lengo la kuongeza ufanisi wa michezo tofautri ndani ya ukanda wa Afrika Mashariki.
Dr. Shein alisema hayo katika Hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif wakati akiifungua Michezo ya Majeshi kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwenye uwanja wa Amani Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar alisema kwa kipindi kirefu sasa majeshi ya Afrika Mashariki yamekuwa yakitoa mchango muhimu wa kupata wachezaji wa michezo mbali mbali wakati wanapoziwakilisha nchi wanachma katika mashindano ya Kimataifa.
Alisema baadhi ya Timu za Majeshi katika ukanda wa afrika Mashariki ndizo zinazotoa upinzani mkubwa katika mashindano ya Kitaifa na baadhi yao kuwa mabingwa na kuziwakilishi nchi hizo Kimataifa.
“Wapiganaji wetu wameendelea kuwa wshiriki wazuri katika michezo ya riadha, mbio za Baskeli, kuogelea na michezo mengine “. Alisema Dr. Shein.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi alivipongeza vikosi vyote vya ukanda huu kwa kuzingatia umuhimu wa michezo kwa wapiganaji wao na kuweza kuziwakilisha nchi zao kimataifa.
Aliwanasihi wanamichezo hao majeshi kuendelea na utaratibu wao wa kuifanya michezo kuwa ni miongoni mwa mambo muhimu yanayopaswa wayaendeleze katika vikosi vyao.
Dr. Sheni alitoa wito kwa timu shiriki kwenye mashindano hayo kuweka mikakati kwa kuwaandaa wanamichezo wazuri ambao wataziwakilisha vyema nchi hizi katika mashindano ya kimataifa na kuleta ushindi wa medali tofauti.
Hata hivyop Dr. Sheni alisema kwamba zipo changa moto zilizosababisha Timu za Ukanda wa Afrika mashariki kutokufanya vizuri katika michezo yua madola ilioyomalizika kwenye Mji wa Glasgow huko Uindereza.
Rais Shein aliwapongeza wanamichezo wa Kenya ambao wamefanya vyema kwenye mashindano hayo na kuiosha uso Afrika ya mashariki kwa kurudi na medali nyingi kwenye mashindano hayo.
Alisisitiza umuhimu wa kuandaliwa kwa utaratibu maalum kwa wanamichezo wa majeshi ambao ndio weledi wakubwa katika fani ya michezo mbali mbali kupewa nafasi ya kueneza ujuzi na maarifa yao kwa rais, wafanyakazi wa taasisi za umma pamoja na wanafunzi maskulini.
Alifahamisha kwamba utaratibu huo unaweza kusaidia kupata vipaji vya riadha na michezo mengine kwa wananchi walioko uraiani.
Alieleza kuwa michezo huimarisha ushirikiano na kuleta burdani na furaha mambo ambao ni muhimu hasa kwa watu wanaosimamia na kuyatekeleza majukumu mazito kama ya ulinzi.
Alisema kupitia medani ya michezo majeshi hayo ya afrika mashariki yanaweza kuimarisha uhusiano na kuangalia maeneo mengine mapya ya kushirikiana ili kuzidi kuyamudu vyema majukumu yao.
Alitoa wito kwa majeshi hayo kuityumia fursa hiyo ya michezo katika kubadilishana uzoefu na mbinu mbali mbali za kukabiliana na changamoto zinayoyakabili majeshi hayo wakielewa kwamba wana dhamana ya kusimamia amani na usalama wa wananchi wa afrika mashariki na kuhakikisha ukanda huu ni wenye amani ya kudumu.
No comments:
Post a Comment