Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea shada la maua kutoka kwa Ndugu Juster Mutakyawa mara baada ya kuwasili kwenye ofisi ya ubalozi wa Tanzania nchini Marekani iliyoko Washington tarehe 3.8.2014.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akipokewa na Mwenyekiti wa kikundi cha wanawake wajasiriamali cha Watanzania wanaoishi Washington kiitwacho TANO Ladies Ndugu Asha Hariz wakati alipotembelea ofisi ya ubalozi wa Tanzania nchini Marekani tarehe 3.8.2014

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea kipeperushi kutoka kwa Rais na Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Help for Underserved Communities (HUC) ya nchini Marekani Ndugu Zawadi Sakapalla baada ya kupata taarifa ya huduma mbalimbali zitolewazo na kampuni hiyo. Kampuni hiyo husaidia familia maskini kwa kuwapatia huduma ya maji safi na salama kwa kuwachimbia visima pamoja na kutoa vifaa vya elimu kwa wanafunzi.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na akina mama wa kitanzania wajasiriamali wanaoishi nchini Marekani kwenye ukumbi wa ofisi ya ubalozi wetu mjini Washington tarehe 3.8.2014.
Baadhi ya wanawake wajasiriamali na wafanyakazi wa ubalozi wa Tanzania nchini Marekani wakisikiliza kwa makini hotuba iliyokuwa ikitolewa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
PICHA NA JOHN LUKUWI.
No comments:
Post a Comment