Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, August 12, 2014

MAMIA YA WANANCHI WAFURIKA JIJINI DAR KWA NABII ANAYEDAIWA KUPONYA WATU UKIMWI, MSANII MMOJA WA FILAMU ATOA USHUHUDA JINSI ALIVYOPONA

Nabii Samwel Mahela  wa Kanisa la Pentecostal Power Ministry (PPM) lililopo Mikocheni A (katikati mwenye suti), akitoa huduma ya maombezi katika kanisa hilo.
MSANII wa Filamu aliyejitambulisha kwa jina moja la Jane amedai amepona ukimwi baada ya kuombewa katika Kanisa la Pentecostal Power Ministry (PPM) lililopo Mikochezi A.

Akizungumza mbele ya waumini wa kanila hilo Dar es Salaam mwanzoni 



mwa wiki hii wakati akitoa ushuhuda wa kupona ugonjwa huo alisema ana mshukuru mwenyezi mungu na Mchungaji kiongozi wa Kanisa hilo Nabii Samweli Mahela kwa kumuombea na kupona.


"Nampashukurani zangu mungu kwa kuniponya kupitia mtumishi wake Nabii Mahela nimeteseka sana na ugonjwa huu aleluya sasa nimepona"alisema Jane na kushangiliwa na waumini wa kanisa hilo.

Jane alisema alianza kuugua ugonjwa huu zaidi ya miaka 10 iliyopita na kupata matibabu katika hospitali mbalimbali bila kupata nafuu mpaka alipoambiwa na mmoja wa waumini wa kanisa hilo aliyemtaja kwa jina la Onesmo kuwa kuna watu wanapona baada ya kuombewa katika kanisa hilo na Nabii Mahela.

"Baada ya kuambiwa kuhusu uponyaji huo nilifika kanisani hapa na kuonana na Nabii Mahela ambaye alinifanyia maombi mfululizo na kuona hali yangu ikibadilika na sasa afya yangu imeimarika" alisema Jane.

Akizungumza  kuhusu suala hilo Nabii Mahela alisema mbele za mungu hakuna lisilo wezekana kama ilivyowezekana kwa Jane kwa kuwa aliamini atapona kwa maombi na kweli amepata nafuu jambo la kumshukuru mungu.

"Biblia inasema kila aaminie atapona kwa jina la kristo na ndivyo ilivyotokea kwa Jane" alisema Nabii Mahela.

No comments:

Post a Comment