Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, August 18, 2014

MANCHESTER CITY WAANZA LIGI KUU ENGLAND KWA KUIFUMUA 2-0 NEWCASTLE UNITED

Mnyumbulikaji wa Kihispania: David Silva akifunga bao la kuongoza
MABINGWA watetezi wa ligi kuu soka nchini England, Manchester City wameanza vyema kampeni za kutetea taji lao baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 ugenini dhidi ya Newcastle United katika dimba la St. James Park.
Bao la kwanza la Man City katika mechi hiyo iliyomalizika dakika chache zilizopita limefungwa na kiungo mshambuliaji, raia wa Hispania, David Silva katika dakika ya 39' akimalizia vizuri pasi ya Edin Dzeko.
Mshambuliaji hatari wa Argentina, Sergio Kun Aguero aliifungia City bao la pili katika dakika za nyongeza.
Huu ni mwanzo mzuri kwa kocha Manuel Pellegrini mwenye kibarua kizito cha kulibakisha kombe Etihad mbele ya makocha wenzake wa kiwango cha dunia akiwemo Louis Van Gaal (Manchester United), Jose Mourinho (Chelsea), Brendan Rodgers (Liverpoool) na Aserne Wenger (Asernal).

 
Kikosi cha Newcastle: Krul, Janmaat, Williamson, Coloccini, Dummett, Colback, Anita (Obertan 63), Sissoko, Cabella, Gouffran (Aarons 74), Riviere (Perez 84).

Wachezaji wa akiba: Haidara, Elliot, Steven Taylor, Abeid.
Kikosi cha Man City: Hart, Clichy, Demichelis, Kompany, Kolarov, Fernando, Toure, Nasri (Milner 78), Jovetic (Fernandinho 73), Silva, Dzeko (Aguero 83).

Wachezaji wa akiba: Zabaleta, Caballero, Jesus Navas, Boyata.
Kadi za njano: Silva, Demichelis, Kolarov, Kompany.
Mwamuzi: Martin Atkinson (W Yorkshire)

No comments:

Post a Comment