Mashabiki 21 wa Westham na Newcastle wamekamatwa na polisi mjini Dusseldorf (picha ya juu haihusiani na tukio).
POLISI
nchini Ujerumani wamewatia mbaroni mashabiki 21 wa klabu za Westham na
Newcastle baada ya kuanzishaji fujo na kuzichapa 'kavukavu' huko
Dusseldorf.
Mapigano hayo yalizuku baina ya mashabiki hao hasimu jana mchana na polisi 100 walipelekwa eneo la tukio kutuliza ghasia.
Msemaji wa polisi wa Polizeipräsidium Düsseldorf alisema:
"Kulikuwa na mashabiki 300 wa Uingereza katikati ya mji".
"Mashabiki
kutoka klabu zote walikutana na awali ya yote walikuwa na bia na
walipokutana walianza kurushiana maneno na baadaye kuamua kupigana".
"Tulituma
polisi 100 katikati ya mji ili kutuliza mambo na zoezi hilo
lilifanikiwa haraka na kwa muda mfupi tuliwatia mbaroni mashabiki 21",
Mwishoni mwa wiki hii klabu za Newcastle na West Ham zinachuana katika kombe la Schalke 04 .
CHANZO BARAKA MPEJA
No comments:
Post a Comment