Mchezaji kutoka Cameroon Albert Ebosse amefariki dunia baada
ya kurushiwa kitu na mashabiki katika mchezo wa ligi nchini Algeria.
Ebosse, 24, alithibitishwa kuwa amefariki baada ya
kufikishwa hospitali katika eneo la Tizi Ouzou, mashariki mwa mji mkuu,
Algiers.
Mshambuliaji huyo wa klabu ya JS Kabylie, ambaye alikuwa
amefunga goli moja katika mchezo huo
waliopoteza kwa 2-1, dhidi ya USM Alger
aligongwa na kitu hicho baada ya mpira kumalizika, wakati wachezaji wakiwa
wanatoka uwanjani.
Wizara ya mambo ya ndani ya nchi imetaka uchunguzi kufanyika
mara moja.
Haijathibitishwa ni kitu gani hasa alichogongwa nacho,
lakini gazeti moja la Algeria limesema mashabiki walikuwa wamekasirishwa na
kufungwa na walikuwa wakirusha mawe.
Taarifa iliyotolewa na klabu yake imesema :"alikufa
kutokana na jeraha la kichwani" baada ya kurushiwa kitu mwisho wa mchezo.
Rais wa shirikisho la kandanda barani Afrika, Issa Hayatou
ametoa taarifa inayolaani tukio hilo.
No comments:
Post a Comment