Msanii nyota wa muziki wa kizazi kipya, Ambwene Yesaya ‘AY’ akipozi
. Ambwene Yesaya ‘AY’ ameanika siri za Ikulu ya Rais Baraka Obama wa Marekani, baada ya kuitembelea wakati alipokwenda kwa ajili ya shoo akiwa na wenzake tisa kutoka Afrika.
“Nilipokwenda sikumkuta Rais Obama, alikuwa Minnesota kwa mambo yake, lakini tulipokelewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ed Royce ambaye pia alihudhuria shoo yetu. Pale tulipewa ‘brief’ kidogo na mambo mengine yakaendelea,”alisema AY.
Alisema wakati wa mazungumzo yake na Royce, kiongozi huyo alimwambia Marekani imekuwa ikitoa fedha nyingi kwa viongozi wa Afrika, lakini zinatumika ndivyo sivyo, hivyo hivi sasa inafikiria kubadili uelekeo ili iwe inatoa msaada zaidi kwa wasanii wakiamini wanaweza kufikia malengo yao.Alisema pia alipata muda wa kubadilishana mawazo na mabosi wa Benki ya Dunia na wale wa shirika la misaada la Marekani, USAID.
Rais Baraka Obama wa Marekani akizungumza jambo.
Katika shoo yao iliyofanyika New Seum, Washington, DC, watu mbalimbali walihudhuria akiwemo nyota wa muziki wa Afrika mwenyeji wa Senegal, Akon.AY alikuwa mmoja wa wasanii hao tisa waliochaguliwa kutoka nchi 11 za Afrika, waliokwenda katika ziara hiyo iliyoandaliwa kwa pamoja kati ya Ikulu ya Marekani na shirika la One Organization.
No comments:
Post a Comment