Pages

Thursday, August 28, 2014

MTOTO AGONGWA NA GARI NA KUFARIKI VWAWA MBEYA

Mtoto mwenye umri wa miaka 09 aliyefahamika kwa jina la Nelly Alick mkazi wa Mlolo amefariki muda dunia muda mfupi wakati anapatiwa matibabu katika hospitali ya wilaya ya Mbozi baada ya kugongwa na gari lenye namba za usajili T.257 CRP aina ya Toyota Noah lililokuwa likiendeshwa na Lameck Madihan (34) mkazi wa Mlolo. 



Ajali hiyo imetokea jana majira ya saa 09:30 alasiri huko maeneo ya Karasha, kata na tarafa ya Vwawa, wilaya ya Mbozi, mkoa wa Mbeya katika barabara ya Mbeya/Tunduma. Chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi. Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya wilaya Mbozi. Dereva amekamatwa na gari lipo kituoni. 
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Ahmed Z. Msangi anatoa wito kwa madereva kuwa makini wanapotumia vyombo vya moto ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika. Aidha, anatoa wito kwa watembea kwa miguu kuwa makini wanapotumia barabara ili kuepuka madhara yanayoweza kuepukika.

No comments:

Post a Comment