Mumewe Meriam ni raia wa Marekani
Mwanamke wa Sudan aliyetoroka kutoka nchini humo baada ya
kunusurika hukumu ya kifo kwa kosa la ‘kuasi dini ya kiislamu’,Meriam Yahia
Ibrahim Ishag, amewasili Marekani.
Alihukumiwa kunyongwa mapema mwaka huu lakini baadaye
akaachiliwa huru mwezi Juni baada ya ulimwengu mzima kukemea uamuzi huo
uliotolewa na mahakama moja nchini humo.
Babake Bi. Ibrahim ni muislamu na hivyo basi inavyoambatana
na sheria za kiislamu za Sudan Bi. Meriam pia ni muislamu na hawezi kuasi dini
ya kiislamu.
Lakini Meriam amesisitiza kuwa hajawahi kuwa muumini wa dini
ya kiislamu kwani alilelewa na mamake ambaye ni Mkiristo.
Kufuatia malalamiko kutoka kote ulimwenguni, aliachiliwa
huru mwezi Juni. Bintiye Meriam, Maya, alizaliwa gerezani mwezi Mei. Baada ya kuachiliwa
kutoka gerezani, Meriam alizuiliwa kutoka nchini Sudan na familia yake
ikalazimika kutafuta hifadhi katika ubalozi wa Marekani uliopo Khartoum.
Bi. Ibrahim aliwasili Philadelphia kwa ndege Alhamisi jioni
kutoka Rome, Italia akiwa na mume wake wa kimarekani.
Mumewe Bi Meriam, Daniel Wani, pia ni muumini wa kikiristo
na pia ni mzaliwa wa Sudan kusini lakini ana uraia wa kimerakani.
Meriam aliponea kifo baada ya mahakama kubatilisha uamuzi wa
kumnyonga kwa kuasi dini
Meriam alikaribishwa kwa njia ya kipekee alipopitia
Philadephia na kutajwa kuwa “mpigania uhuru wa kimataifa’ na mayor wa
Philadelphia, Michael Nutter. Nutter pia alisema watu watakumbuka Meriam kama
‘wengine waliotupigania kuwa huru,’ na kumlinganisha Meriam na Rosa Parks.Rosa
Parks alisifika na kutazamwa kuwa ushujaa wa harakati za haki za kiraia nchini
Marekani alipokataa kuondokea mwanamme mzungu kitini wakiwa ndani ya gari huko
Alabama.
Hatimaye Nutter alimkabidhi Meriam mfano wa ‘kengele ya
uhuru,’ ishara ya uhuru wa Marekani. Aidha, kwa mujibu wa msemaji wa Vertican,
Bi Meriam akiwa Rome alikutana na papa ‘aliyemshukuru kwa kuwa imara katika
Imani yake.”
Safari ya Bi Meriam ilifikia kikomo New Hampshire kwani
alikuwa anasubiriwa kwa hamu na ghamu na jamaa na wafuasi wake katika uwanja wa
ndege.
Alipoondoka Sudan alipitia Italy ambako alikutana na Papa
Francis
Kwa mujibu wa mwanahabari wa BBC aliyeshuhudia tukio hilo,
Meriam alikaribishwa na halaiki ya watu, wengine wao wakiimbia “Marekani iishi
milele.”
Aidha mwanahabari wetu alituarifu kuwa mume wa Bi Meriam
alitoa hotuba fupi na kushukuru serikali ya Marekani na maseneta wa New
Hampshire kwa kumpigania na kwa kufanya mipango ya kumpa mke wake hifadhi. Pia
alishukuru watu wa Sudan kwa usaidizi wao.
Familia ya Meriam inakusudia kuishi New Hampshire kwani
jamaa wa mume wake wako huko.
No comments:
Post a Comment