Pages

Monday, August 11, 2014

NYUMBA YA MWANAUME ALIYEKUWA AKIWALAWITI WATOTO WA KIUME HUKO MOSHI YATEKETEZWA KWA MOTO NA WANANCHI WENYE HASIRA KALI


Wananchi wenye hasira, wameteketeza kwa moto nyumba ya mkazi wa Kijiji cha Mwika Uuwo, Wilaya ya Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro, wakimtuhumu kulawiti wanaume  wenzake. Hasira za wananchi hao zilifikia kiwango kisichohimilika baada ya mtuhumiwa huyo mwenye umri wa miaka 42, kudaiwa kumlawiti mtoto wa  kiume mwenye umri wa miaka 12 kijijini hapo juzi.Wananchi wa kijiji hicho wanamtuhumu mwanamume huyo ambaye jina lake tunalihifadhi kwa sasa kwa sababu za kitaaluma, kuwa ana tabia ya kuwalawiti vijana kijijini hapo.Habari kutoka kijijini hapo zilizothibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz, zilisema kuwa mbali na kuchoma moto nyumba hiyo, pia walifyeka ekari moja ya shamba la migomba la mtuhumiwa huyo.





Kamanda Boaz  alisema   jana kuwa tukio la  kuchomwa moto kwa nyumba hiyo lilitokea saa 3:30 usiku na ilipofika saa 6:00 usiku wa kuamkia jana, nyumba hiyo ilikuwa imeteketea  yote.




 Kwa mujibu wa Kamanda Boaz, wakati wananchi wakiiteketeza nyumba hiyo na kufyeka shamba lake la migomba, mtuhumiwa huyo anayetafutwa na polisi hakuwepo ndani ya nyumba hiyo.





“Siyo jambo jema kuchukua sheria mkononi kwa sababu huyu ametenda kosa halafu mnaokwenda kuchoma nyumba yake, nanyi pia mnatenda kosa la jinai,”alisema Boaz.




“Kama walijua (wananchi) kuwa huyo mtuhumiwa amerudi na yuko ndani, wangemkamata na kumfikisha polisi siyo kuchoma nyumba. Nchi lazima iendeshwe kwa misingi ya kisheria,”alisisitiza.



Kamanda Boaz alisema kuwa  juzi polisi walifika kumtafuta mtuhumiwa huyo kwa lengo la kumkamata, lakini hawakuweza kumpata na inadaiwa  alikuwa amekimbilia mahali kusikojulikana.

No comments:

Post a Comment