Pages

Friday, August 22, 2014

PICHA NA HABARI;;;MAMA AMCHANA MWANAWE WA MIEZI MIWILI NA VIWEMBE

BI ANASTAZIA NGILITU AKIWA NA MWANAYE AMBAYE ALIMCHANA KWA VIWEMBE KUPATA SEHEMU YA HAJA KUBWA.

MWANDISHI NA MMILIKI WA KIJUKUU BLOG WILLIAM BUNDALA KUSHOTO AKIFANYA MAHOJIANO NA ANASTAZIA NGILITU JUU YA MAISHA YAKE NA SAKATA HILO LA KUMCHANA MTOTO WAKE.

 
MAHOJIANO YAKIENDELEA
TITI LA KUSHOTO LA ANASTAZIA NGILITU LINALOSUMBULIWA NA UVIMBE

HAPA NIKIFANYA MAHOJIANO NA MAMA IVAN ALIYETAJWA KUWA MSAADA MKUBWA KWA ANASTAZIA NGILITU KIPINDI CHOTE CHA MATATIZO.

BI ANASTAZIA NGILITU AKIWA NA MWANAE AKIMNYONYESHA TITI MOJA SIKU ZOTE HALI INAYOPELEKEA MAZIWA KUISHA NA KULAZIMIKA KUMNYWESHA MAJI NA CHAI MTOTO WA MIEZI MIWILI.

ANASTAZIA AKIWA NA MTOTO WAKE.
HAPA NILIMUULIZA SWALI AMBALO LILIMTOA MACHOZI,NI KUHUSU WATOTO WAKE WENGINE WAKO WAPI? ALILIA SANA KABALA YA KUJIBU HAJUI HATA KAMA WAKO HAI AU LAA.

MAHOJIANO YAKIENDELEA.

MWONEKANO WA MASIKIO YAKE BAADA YA KUVUTWA HELENI NA MUMEWE WA KWANZA.

NI MAMA MWENYE AFYA KABISA,ILA MAISHA NA MATESO NDIYO YANAMFANYA AWE OMBAOMBA.



MWANZA

Vitendo vya baadhi ya wananchi kujitibu pasipo kufuata maagizo na njia za kitaalamu vimeendelea kukithiri nchini ambapo hapa jijini Mwanza mama mmoja ameamua kumchanja kwa viwembe mwanae mwenye umri wa wiki mbili baada ya 

mtoto huyo kuzaliwa akiwa hana sehemu ya Haja kubwa.



Tukio hilo limetokea hivi karibuni baada ya mama huyo aliyefahamika kwa jina la Anastazia Ngilitu kumchana kwa wembe zaidi ya mara tatu ili kumsaidia mwanae kupata haja kubwa kwa kile kilichodaiwa mtoto huyo kuzaliwa akiwa hana sehemu 

ya haja kubwa.




Akiongea na Kijukuu Blog mama huyo mkazi wa Tabora aishie jiini mwanza kwa sasa amesema kuwa alijifungua watoto mapacha watatu ndani ya Mtaro kisha wawili kufariki alipofikswa Hospitali na kusalia mtoto mmoja aliyekutwa na tatizo la 

na sehemu ya haja kubwa.




Sambamba na hayo mama huyo amesema kuwa sababu za kumchana na wembe mwanawe ni baada ya kumuona mtoto wake anashindwa kupata haja kubwa hali 

iliyopelekea tumbo kujuaa na kulia.




Ameongeza kuwa wakati wa kujifungua mtoto huyo walimfanyia upasuaji katika hospitali ya Bugando ila hali ya kuziba ilijirudia tena na kuamua kumchana kwa 

kutoakana na kutokuwa na uwezo wa kulipia gharama za upasuaji hospitali.




Katika hatua nyingine Mama huyo amesema kuwa kwa sasa hali yake ya Maisha siyo nzuri kwani watoto wake wanaishi kwa kunywa maji na kwamba hapo awali alikuwa anafanya kazi ya kufua nguo kwenye nyumba za watu ila kwa sasa hawezi 

kutokana na kuwa na motto mdogo.




Sambamba na hayo mama huyu anasema kuwa licha ya kuolewa na wanaume watatu kwa wakati tofauti na kila mmoja kumnyanyasa kwa kumpiga na mwingine kumdhurumu pesa zaidi amesikitishwa na kitendo cha Mume wake wa sasa hivi kumtaka kufanya mapenzi ikiwa tumbo la uzazi halijakaza hali anayotaja kumsababishia maumivu makali na kutokwa na damu nyingi baada ya mumewe 

kumpiga.




Kitendo cha mama huyu kumchana mtoto wake kwa wembe kinatoakana na hofu ya kwenda hospitali kwani anasema hana uwezo wa pesa kwani kwa sasa yeye mwenyewe anasumbuliwa na uvimbe katika titi lake la kushoto na alipoenda Hospitali ya SEKOTURE aliambiwa gharama za upasuaji ni shilingi elfu 30 na 

alipokosa alirudi nyumbani na kuendelea kujitibu kwa dawa za kienyeji.




Kwa upande wao baadhi ya kina majirani ambao wamekuwa wakimpa msaada mama huyu mara kwa mara,Wameiambia KIJUKUU BLOG kuwa mama huyu ana maisha magumu kwani mume wake humpiga na kumfukuza mara kwa mara hali inayomfanya aishi kwa kuomba omba na wakati mwingine kulala na watoto wake 

bila kula.




Taarifa za awali zinaonyesha kuwa mama huyu aliolewa na mume wa kwanza mkazi wa eneo la maji moto mkoani Mara na waliachana baada ya kupigwa na kuchomwa kisu tumboni ikiwa ni pamoja na kupigiliwa msumali wa nchi sita katikati ya mkono 

wake wa kushoto ikiwa ni sambamba na kumvuta hereni akimwambia kuwa ni dalili za kuwa malaya hali iliyomsababibishia masikio yake kuvimba.




Mume wa pili aliyemuoa mama huyo inaelezwa kuwa yeye alimdhurumu kiwanja walichouza milioni moja na laki saba kilichokuwa eneo la makaburi Bwiru kisha 

kuzichukua na kuaga kwenda kuzifanyia biashara.




Kuhusu ndugu Bi Anastazia amesema kuwa wazazi wake wote wamefariki na kwamba aliyebaki ni bibi yake ambaye naye anamtaja kuwa ni mchawi kwani wakati alipoenda Tabora,bibi yake alimwambia ampe mkono wa mtoto ili usiku wa manane 

amuamshe kwa kumpiga nao kichwani ili aende kazini.




Anastazia anasema kuwa kutokana na matatizo hayo aliwahi kushauriwa kumtupa mtoto huyo eneo la vichakani soko la sabasaba,ushauri aliopewa na rafiki yake mkazi wa Ilemela aliyemtaja kwa jina moja la Amina ambaye alimwambie mtoto wako hatapona,Jambo ambalo yeye alikataa na kusema kuwa anaogopa mkono wa Sheria.




Tatizo linalomsumbua mama huyo kwa sasa ni chakula na matibabu kwa mwanaye na yeye mwenyewe anayesumbuliwa na uvimbe katika titi la kushoto na kuwaomba wasamalia wema kumsaidia ili aendelee na shughuli zake aondokane na 

kuombaomba.





NDUGU MSOMAJI KAMA UNATAKA KUMSAIDIA MAMA HUYU NA KUWASILIANA NAYE WASILIANA NA NAMI KWA NAMBA+255 767 942 570
CHANZO KIJUKUU BLOG

No comments:

Post a Comment