Mkuu
wa Kikosi cha Kupambana na Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa akionesha
Cocaine zilizokuwa zimefichwa katika mkanda wa suruali aliyokuwa amevaa
raia wa Colombia, Andres Filipe Ballesteros Uribe (28), mara baada ya
kukamatwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini
Dar es Salaam. Picha zote na Francis Dande.
Baadhi ya dawa alizokuwa amemeza mtuhumiwa huyo.
Hati ya kusafiria ya mtuhumiwa huyo yenye namba AP816263 iliyotolewa Julai 3,2014 nchini Columbia.
Suruali ya mtuhumiwa huyo ikiwa imezungushiwa Cocaine.
Baadhi ya dawa alizokuwa amemeza mtuhumiwa huyo.
Hati ya kusafiria ya mtuhumiwa huyo yenye namba AP816263 iliyotolewa Julai 3,2014 nchini Columbia.
KIKOSI
cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini kinamshikilia Andres
Filipe Ballesteros Uribe (28) raia wa Colombia kwa tuhuma za kuingiza
dawa hizo nchini kinyume cha sheria.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo, Mkuu wa kikosi hicho,
Kamanda Godfrey Nzowa alisema mtuhumiwa huyo aliingia nchini saa nane
usiku kwa ndege ya shirika la Ethiopian akitokea Adisi Ababa.
Alisema mtuhumiwa huyo alikutwa na Cocaine iliyofungwa kwenye pakiti sita tofauti na kuiwekasehemu za siri, kiunoni kama mkanda na nyingine tumboni.
Kamanda
Nzowa alisema mtuhumiwa huyo mwenye pasi ya kusafiria namba AP816263
iliyotolewa Julai 3,2014 nchini Columbia, alitoka Columbia kupitia Adis
Ababa kuja Tanzania huku akibainisha kwamba hiyo ni njia mpya ya
usafirishaji wa dawa hizo haramu.
“Hawa
jamaa wanajaribu kubuni mbinu mpya kama huyu kijana alikuwa amefunga
unga wa cocaine kama zilivyokuwa zikifungwa pipi na akazimeza… mpaka
sasa ameshatoa pipi 13 kwa njia ya haja kubwa na anaendelea kutoa.
“…Sio
rahisi kujua idadi ya mzigo aliokuwa nao mpaka atakapomaliza kuzitoa
zote za tumboni ndiyo tunaweza kusema uzito wa dawa hizo na thamani
yake,” alisema kamanda Nzowa.
Alisisitiza
kwamba taarifa sasa wanazopeana kwenye mtandao wao unawezesha kukamatwa
kwa watuhumiwa huku akibainisha kuwa lengo ni kudhibiti usafirishaji
kwa njia yoyote.
Kamanda
Nzowa alisema mafanikio yanaonekana kwa vile kuanzia Juni 24 mwaka huu
hadi Agosti 10 hakuna mtu aliyekamatwa akiingiza huku akibainisha kwamba
umadhubuti wa mtandao wao umefanikisha hilo.
“Asiyeamini
kwamba tumefanikiwa atujaribu aone… naamini tunakokwenda dawa za
kulevya hasa cocaine na heroine zitakuwa hazipiti wala kuingia
Tanzania,” alisema na kuongeza kwamba wanadhibiti pia ulimaji wa bangi.
Kwa mujibu wa kamanda huyo lengo la mtandao wao ni kudhibiti sio kukamata wala kuteketeza.
No comments:
Post a Comment