Pages

Friday, August 29, 2014

RONALDO ABEBA TUZO YA MWANASOKA BORA ULAYA


Ronaldo akimkabidhi tuzo yake ya Mwanasoka Bora wa Dunia, Rais wa Real Madrid, PerezMRENO Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Ulaya msimu wa 2013-2014 katika sherehe zilizofanyika jioni ya leo mjini Monaco, Ufaransa.Nyota huyo wa Real Madrid amewapiku nyota wa Bayern Munich, kipa Mjerumani Manuel Neuer na winga Mholanzi, Arjen Robben alioingia nao 

 
fainali.  Wakati Neuer alishinda taji la Bundesliga na Kombe la Dunia msimu uliopita, Robben alifunga mabao 22 kwa klabu na timu yake ya taifa msimu uliopita na Ronaldo alifunga mabao 56 na kutoa pasi 15 za mabao Real Madrid na Ureno. Mshindi wa mwaka jana, Mfaransa Franck Ribery hakuingia fainali.

Ronaldo pia ni Mwanasoka Bora wa Dunia na ushindi huu ni pigo lingine kwa mpinzani wake mkubwa, Lionel Messi wa Argentina na Barcelona.

No comments:

Post a Comment