MWANASHERIA wa Luis Suarez anajiamini kuwa adhabu ya kifungo
cha miezi minne cha mshambuliaji wa Barcelona, Luis Suarez itapunguzwa na
mahakama ya juu ya rufani ya michezo ya CAS ambapo rufani hiyo itasikilizwa
kesho ijumaa.
Suarezi alikata rufaa kupinga adhabu ya kufungiwa shughuli
zote za soka na FIFA na rufani yake
itasikilizwa Agosti 8 mwaka huu katika
mahakama hiyo iliyopo Lausananne, Uswizi.Nyota huyo mwenye miaka 27 alifungiwa
baada ya kumng’ata beki wa Italia,Giorgio Chiellini wakati akiichezea Uruguay
katika mechi ya kombe la dunia nchini Brazil na baada ya tukio hilo alijiunga
na Barcelona kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 75 kutokea Liverpool.
No comments:
Post a Comment