Pages

Saturday, August 23, 2014

SENEGAL YAFUNGA MPAKA KUHOFIA EBOLA

Senegal imefunga mpaka wake na Guinea kwa sababu ya kuzuka kwa ugonjwa wa Ebola, licha ya onyo kuwa hatua hiyo haisaidii.
Senegal pia imepiga marufuku ndege na meli kutoka Guinea, Liberia na Sierra Leone, nchi tatu ambazo zimeathirika sana na ugonjwa huo.

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema kupiga marufuku usafiri hakusaidii, hasa ikiwa hatua hiyo itazuia madaktari kusafiri kwenda kukabiliana na tatizo hilo.
Mji mkuu wa Senegal, Dakar ni kitovu cha mawasiliano kwa nchi za Afrika Magharibi.
Madaktari wengi pamoja na dawa zinazowasili kutoka Ulaya na Marekani hupitia mjini Dakar kabla ya kuelekea katika nchi zilizoathirika.

Siku ya Alhamisi, Afrika Kusini ilipiga marufuku raia kutoka nchi tatu za Afrika Magharibi zilizoathirika na Ebola kuingia Afrika Kusini, na pia raia wa nchi hiyo kwenda Afrika Magharibi kwa safari zisizo za lazima

No comments:

Post a Comment