Kocha wa Atletico Madrid Diego Simeone amefungiwa mechi nane kwa utovu
wa nidhamu alioonesha kwenye mechi ya Spanish Super Cup. Simeone, 44,
alimgusa mmoja wa waamuzi kisogoni katika mechi iliyokuwa imejaa hamasa
kati ya Atletico Madrid na Real Madrid, ambapo Atletico walishinda 2-1.
Shirikisho la soka la Spain (RFEF) limethibitisha kuwa adhabu hiyo ni ya
makosa manne tofauti. Kocha msaidizi German Burgos atasimamia mechi za
Attletico wakati wa adhabu hii.
No comments:
Post a Comment