Pages

Saturday, August 16, 2014

Taarifa Kwa Umma Kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchiwa Tanzania (JWTZ) Kuhusu Kuzindua Huduma ya Tiba bure kwa jamii

Jeshi la Ulinzi la Wananchiwa Tanzania (JWTZ), linatarajia kuzindua huduma ya Tiba kwa jamii kuanzia tarehe 15 Agosti 2014 hadi 19 Agosti 2014 kuanzia saa 12:00 asubuhi hadi 12:00 jioni katika viwanja vya Mnazi mmoja. Huduma hizi zinakwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 50 ya JWTZ.


Huduma zitakazotolewa ni pamoja na vipimo vya magonjwa ya Homa ya Ini (Hepatitis B& C), Presha, Kisukari, Huduma za Ushauri nasaha na kupima VVU, Huduma za uchangia damu salama, Macho, Kinywana Koo. Kwa vipimo vya Malaria, matibabu yatatolewa hapo hapo. Huduma zote hizo ni bure.
Nafasi hii itatoa mwanga wakuweza kuona ueledi wa madakitari wetu wazalendo ambao ni matunda yenu.
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo anatarajiwa kuwa Waziri wa Afya Dk. Selemani Seif Rashidi. JWTZ linawakaribisha wananchi wote.

Tumelinda, tunalinda, tutalindadaimaTaifaletu Tanzania.


Imetolewa na
 Kurugenzi ya Habari na Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P 9203,
 Dar es Salaam, Tanzania.
Kwa Mawasiliano zaidi: 0754 - 270136

No comments:

Post a Comment