DEREVA wa Basi la
Kampuni ya Usafiri Dar es Salaam (UDA) ambaye hakuweza kufahamika jina lake
mara moja, amejikuta akipewa kibano hevi na askari wa usalama barabarani
‘trafiki’ baada ya kuleta ubabe wakati alipotakiwa kutii sheria bila
shuruti.Tukio hilo la aina yake lililosababisha usumbufu kwa abiria wa basi
hilo, lilitokea juzi Bamaga-Mwenge jijini Dar kufuatia dereva huyo kukataa
kuegesha pembeni basi hilo lenye namba za usajili T 619 CVP lililokuwa
limevunja sheria ya usalama barabarani.
Dereva huyo akionyesha ubishi wa kutotii maagizo ya
'trafiki'.
Imedaiwa kuwa, basi hilo lilishusha abiria kinyume na sheria
kwenye kituo kisicho rasmi maeneo ya Chuo cha Ustawi wa Jamii, Kijitonyama,
Barabara ya Shekilango.
Chanzo makini kilichoshuhudia tukio hilo kimedai kuwa,
kufuatia hali hiyo ndipo trafiki hao watatu walio makini na kazi yao,
walilisimamisha basi hilo ili kumsomea mashitaka dereva huyo sambamba na
kondakta wake lakini wakaleta ubishi na kutoa lugha chafu kitendo ambacho
trafiki hao walishindwa kukivumilia.
Askari wa usalama barabarani ‘trafiki’ wakimtoa nje dereva
jeuri wa UDA.
“Waliendelea kutoa
lugha chafu, hawakuonesha kutii amri ili waambiwe walichokosea ndipo trafiki
wakalazimika kuwadhibiti kwa kuwafunga pingu baada ya kukataa kutii sheria bila
shuruti, tunawapongeza trafiki hawa kwa kuwataiti,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya trafiki kuwadhibiti wawili hao, mmoja wao alishika usukani, wenzake wakakaa
kwenye viti na kuliendesha basi hilo hadi
Kituo cha Polisi Kijitonyama ‘Mabatini’ kwa ajili ya hatua zaidi za
kisheria.
Wananchi wakishuhudia mkasa huo.
Siku za hivi karibuni kumekuwa na malalamiko kutoka kwa
baadhi ya wananchi kwamba, madereva wa mabasi ya Uda wamekuwa wakivunja sana
sheria kama wao wako juu ya sheria kuliko madereva wengine.
Tunashauri madereva kuwa makini na watiifu pindi wanapokuwa
barabarani ili kupunguza ajali ambazo nyingi kati ya hizo zimekuwa zikitokana
na uzembe wa madereva kwa kutotii sheria za usalama barabarani.
No comments:
Post a Comment