BILIONEA William Henry "Bill" Gates naye ameungana na mastaa mbalimbali katika kupambana na ugonjwa wa Amyotrophic Lateral Sclerosis (ALS), maarufu kama Lou Gehrig kupitia kampeni ya ‘Ice Bucket Challenge’.
Bill Gates amefanya hivyo baada ya kutumiwa kampeni hiyo na mmiliki wa mtandao wa Facebook, Mark Zuckerberg huku naye akiwataka Elon Musk, Ryan Seacrest na Chris Anderson kufanya hivyo.
Video iliyowekwa katika mtandao wa kijamii wa Facebook na kijana Pete Frates wiki mbili na nusu zilizopita imewavutia watu wengi wakiwemo Justin Bieber, LeBron James, Chris Christie and Taylor Swift ambao wamechukua ndoo ya maji baridi kuungana katika kampeni hiyo.
Ugonjwa wa ALS hushambulia seli za mishipa ya fahamu na kupelekea mgonjwa kupata matatizo katika kuongea, kumeza, kupumua na baadaye kupooza. Mpaka sasa watu takribani 30,000 nchini Marekani wana ugonjwa huo.
Kampeni ya ‘Ice Bucket Challenge’ hufanyika kwa watu kutengeneza video zao wakijimwagia ndoo ya maji baridi kichwani kisha kuzituma katika mitandao ya kijamii na kuwataka wenzao kufanya hivyo pia ndani ya masaa 24 au kuchangia dola za Kimalekani 100 kwa Chama cha ALS ambapo mara nyingi watu hufanya vyote (kujimwagia maji na kuchangia fedha).
No comments:
Post a Comment