Chelsea wameanza mazungumzo na mshambuliaji wa QPR Loic
Remy, 27, baada ya Fernando Torres, 30, kwenda AC Milan (Telegraph), kiungo wa
Manchester United Tom Cleverly, 25, anafikiria kwenda Aston Villa kwa pauni
milioni 7, baada ya kuzungumza na nahodha wa zamani wa Man Utd Roy Keane ambaye
sasa ni meneja msaidizi Villa Park (Daily Mirror), meneja mpya wa Crystal
Palace Neil Warnock anataka kumchukua beki wa QPR Armand Traore, 24, kwa pauni
milioni 2.5 (Sun), Arsenal wamepata matumaini makubwa ya kumchukua winga
Alessio Cerci, 27, baada ya rais wa Torino, Urbano Cairo kusema mchezaji huyo
atauzwa kwa bei stahiki (Daily Star), Manchester United wanataka kumsajili beki
Timothy Fosu Mensah, 16, kutoka Ajax (Daily Express), uhamisho wa beki Marcos
Rojo, 24, kwenda Manchester United uko hatarini kutokana na kutopata bado
kibali cha kufanya kazi na pia wakala wa tatu wa uhamisho aliyepo kwenye
mkataba wake (Sun), West Ham wanakaribia kukamilisha uhamisho wa Alex Song, 26,
kutoka Barcelona kwa mkopo (Daily Mail), Birmingham City wanataka kumchukua
Hatem Ben Arfa, 27, kutoka Newcastle kwa mkopo (Newcastle Chronicle),
Manchester United wanahitaji kutoa pauni milioni 5 zaidi kuweza kumsajili
Arturo Vidal kutoka Juventus huku klabu hizo mbili zikiendelea na mazungumzo
kabla ya dirisha la usajili kufungwa Jumatatu (Tuttosport), Benfica wanajiandaa
kutoa pauni milioni 7.9 kumtaka mshambuliaji wa Arsenal Joel Campbell (O Jogo),
Manchester United wamekubali kutoa pauni milioni 14.2 na Ajax kumchukua Daley
Blind (De Telegraaf), Chelsea wako tayari kuongeza juhudi kumfuatilia
mshambuliaji wa Roma Mattia Destro kufuatia kuondoka kwa Fernando Torres (Daily
Mirror). Zimesalia siku mbili kabla ya dirisha la usajili kufungwa Jumatatu.
Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Cheers!!!!
No comments:
Post a Comment