Mshambuliaji wa England Danny Welbeck, 23, ameambiwa anaweza
kuondoka Manchester United, wakati Louis van Gaal akiendelea kukisuka kikosi
chake. Tottenham wameonesha nia ya kumtaka Welbeck (Times), mshambuliaji wa
zamani wa Chelsea Samuel Eto'o, 33, amefanyiwa vipimo vya afya Liverpool na
atasaini mkataba wa mwaka mmoja Anfield (Daily Mirror), meneja wa Sunderland
Gus Poyet hajakata tamaa kumsajili mshambuliaji wa
Liverpool Fabio Borini, 23,
na anataka kuchukua wachezaji wengine wawili kwa mkopo (Daily Express),
Barcelona walitoa dau la pauni milioni 48 kumtaka winga wa Real Madrid Angel Di
Maria, 26, lakini ombi hilo lilikataliwa mara moja na rais wa Real Florentino
Perez (sport.es), kiungo wa zamani wa Manchester United Paul Pogba, 21, amefuta
matumaini yoyote ya kurejea Old Trafford baada ya kusaini mkataba mpya wa miaka
mitano Juventus (Daily Star), Liverpool wamemuambia Mario Balotelli kuwa
atapoteza pauni milioni 2 kwa mwaka iwapo ataonesha utovu wa nidhamu, baada ya
pia kukubali kupunguza mshahara wake kutoka AC Milan (Sun), AC Milan wanatazama
kati ya wachezaji sita kuziba pengo la Balotelli, akiwemo Javier Hernandez, 26,
wa Man U, Roberto Soldado, 29, wa Spurs na Fernando Torres, 30, wa Chelsea
(Gazetta dello Sport), Arsenal wanakaribia kumsajili beki wa Olympiakos Kostas
Manolas, 23, kuziba pengo la Thomas Vermaelen aliyekwenda Barcelona (Goal),
kipa wa Stoke City Asmir Begovic, 27, hatoondoka kabla ya dirisha la usajili
kufungwa licha ya Liverpool, Manchester City, Arsenal na Real Madrid kuonesha
dalili za kumtaka (Daily Mirror), AC Milan wanamtaka kiungo wa Chelsea Marco
van Ginkel kwa mkopo (Inside Futbol), boss wa Sunderland Gus Poyet anamtaka
Danny Welbeck wa Man U kwa mkopo (Sunderland Echo), Fredy Guarin anayesakwa na
Man U anajiandaa kujiunga na Zenit St Petersburg baada ya Andre Villas Boaz
kumshawishi mchezaji huyo kutoka Colombia kuhamia Urusi, ingawa lazima kwanza
wafuzu kucheza Champions League (Gazetta dello Sport), Napoli wanafikiria
kumchukua Marouanne Fellaini licha ya kumsajili Jonathan de Guzman (Corriere
dello Sports), mshambuliaji wa Arsenal Lukas Podolski anajiandaa kurejea
Ujerumani na kujiunga na Wolfsburg. Galatasaray na Besitkas wanamtaka mchezaji
huyo, lakini anaonekana kwenda Bundesliga (Metro). Tetesi nyingine kesho
tukijaaliwa. Zimesalia siku tisa kabla ya dirisha la usajili kufungwa. Cheers!!
No comments:
Post a Comment