Manchester City wameacha kumfuatilia kiungo wa Everton Ross
Barkley, 20, baada ya kuambiwa atagharimu pauni zisizopungua milioni 50
(Mirror), Manchester United wanakaribia kumsajili winga wa Real Madrid Angel Di
Maria, 26, na huenda atavunja rekodi ya uhamisho ya Uingereza kwa mkataba wa
pauni milioni 56 (Sky sports), Manchester United pia wamepanda dau kwa mara ya
pili kumwania kiungo wa Juventus Arturo Vidal, 27, katika mkataba
utakaohusisha
Man U kutoa na mchezaji (Star), Mario Balotelli, 24, huenda akawa mchezaji
kamili wa Liverpool katika mkataba wa pauni milioni 16 ifikapo Jumatatu, lakini
Liverpool wameacha kumfuatilia mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Samuel Eto'o,
33, (Liverpool Echo), Eto'o anadhaniwa kudai mshahara wa pauni 100,000 kwa wiki
kutoka kwa Liverpool, lakini sasa inaripotiwa kuwa anafanya mazungumzo na
Everton ingawa kuna timu za Mashariki ya Kati pia zinamtaka (Mirror), Balotelli
hatosaini mkataba wenye kipengele cha utovu wa nidhamu. Mwakilishi wa
mshambuliaji huyo Mino Raiola amedai kuwa mkataba huo hauna tofauti na mikataba
yoyote ya Liverpool na kuwa makubaliano yatafikiwa kabla ya Jumanne (Express),
Arsenal wanafikiria kumchukua Toby Alderweireld, 25, kutoka Atlètico Madrid
kuziba nafasi ya Thomas Vermaelen aliyekwenda Barcelona (Star), Gunners pia
wanamfuatilia beki wa Olympiakos Kostas Manolas, 23, ambaye alichezea Ugiriki
katika Kombe la Dunia na ambaye anatazamwa pia na Man U (Express), kipa wa
Chelsea Petr Cech, 33, anajiandaa kuondoka Darajani baada ya nafasi yake
kuchukuliwa na Thibault Courtois (Mail on Sunday), Lukas Podolski anajiandaa
kuondoka Arsenal na kwenda Juventus kwa mkopo (Sunday Express), Arsene Wenger
alimkataa mara mbili Mario Balotelli anayekwenda Liverpool. Balotelli angeweza
kwenda Emirates kama Wenger angemtaka (Metro), Valencia wanataka kumsajili
Alvaro Negredo kutoka Manchester City kabla ya dirisha la usajili halijafungwa,
pia wanawafuatilia Fernando Llorente na Anthony Martial (Superdeporte).
Zimesalia siku nane kabla ya dirisha la usajili kufungwa. Tetesi nyingine kesho
tukijaaliwa. Cheers!!!
No comments:
Post a Comment