Pages

Wednesday, August 27, 2014

TETESI ZA SOKA ULAYA



Arsenal wapo tayari kutoa dau la pauni milioni 50 kumtaka Edinson Cavani kutoka Paris St-Germain, kutokana na Olivier Giroud kuwa na uwezekano wa kutocheza kwa muda mrefu kutokana na jeraha la mguu (Daily Express), Arsenal pia wanamtaka Danny Welbeck, 23, kutoka Manchester United, kuziba nafasi ya Giroud, lakini Man U wanasita kumuuza Welbeck (Daily Mail), boss wa Arsenal vilevile anataka 


kumchukua kwa mkopo Radamel Falcao, 28, kutoka Monaco, na pia Loic Remy, 27, ambaye anapatikana kwa pauni milioni 8.5 kutoka QPR (the Guardian), boss wa Manchester United Louis van Gaal anafikiria kutaka kumsajili kiungo wa Liverpool Joe Allen, 24, kwa kutoa pauni milioni 20, (Daily Star), United wanafanya mazungumzo ya kumsajili Daley Blind, 24, huku kipa wa zamani wa Man U, Edwin van der Sar akiwa Manchester kukamilisha uhamisho wa beki huyo wa Ajax (Daily Star), Manchester United pia wanafikiria kumtoa Shinji Kagawa, 25, au Javier Hernandez, 26, kama chambo katika mkataba wa kumchukua kiungo wa Juventus Arturo Vidal, 27, (Independent), Real Madrid watatumia kiasi kikubwa cha fedha za mauzo ya Angel Di Maria, kumnunua mshambuliaji wa Monaco, Radamel Falcao (Le Sport), AC Milan wamethibitisha kuwa wanataka kuwasajili Fernando Torres, 30, na kiungo Marco van Ginkel, 21 kutoka Chelsea (Daily Express), AC Milan wamechoka kumsubiri Torres kuamua anataka nini na wamempa makataa, huku wakijiandaa kuanza kumfuatilia Roberto Soldado, 29, kutoka Tottenham au Fabio Borini, 23, wa Liverpool (Inside Futbol), Tottenham wanajiandaa kukamilisha usajili wa beki wa Sevilla Federico Fazio, 27, baada ya kulipa pauni milioni 8 za kipengele cha ununuzi (Daily Telegraph), Spurs pia wanafikiria kumfuatilia kiungo kutoka Cameroon Alexandre Song, 26, ambaye ameambiwa anaweza kuondoka Barcelona bure (the Times), boss wa QPR Harry Redknapp yuko tayari kupanda dau kwa kiungo wa West Ham Mohammed Diame, 27, (Daily Mirror), Alvaro Arbeloa anataka kuondoka Real Madrid kabla ya dirisha la usajili halijafungwa (El Chiringuito), Manchester United wanajiandaa kutoa dau jipya la pauni milioni 33.4 kwa Juventus kumtaka Arturo Vidal (Gazzetta dello Sport), Real Madrid watapambana na Barcelona na Atletico Madrid kutaka kumsajili Marco Reus kutoka Borussia Dortmund (AS), Hatem Ben Arfa anataka kubakia Newcastle licha ya meneja Alan Pardew kutompanga (Newcastle Evening Chronicle), Arsene Wenger anataka kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Birmingham City, Nikola Zigic ambaye ni mchezaji huru (www.zurnal.rs). Share tetesi hizi na wapenda soka wote. Zimesalia siku tano kabla ya dirisha la usajili kufungwa. Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa.Na Salim Kikeke

No comments:

Post a Comment