Boss wa Manchester United Louis van Gaal anajaribu kumnunua
kiungo wa Juventus Arturo Vidal, 27, na beki wa Ajax Daley Blind, 24, kabla ya
dirisha la usajili kufungwa Septemba mosi (Daily Mirror), United watalazimika
kulipa pauni milioni 20 kumsajili Blind (Sun), Liverpool bado wanajaribu
kumfuatilia kiungo wa zamani wa Arsenal Alex Song, 26, ambaye yuko Barcelona
(Metro), meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amesema hatotaka kuwasajili Danny
Welbeck, 23, kutoka Man U, Radamel Falcao kutoka Monaco, 28, na Nikola Zigic,
33, kutoka Birmingham
(London24.com), Manchester United watapanda dau la pauni
milioni 24 kwa kiungo wa Sporting Lisbon William Carvalho, 22, wakati Louis van
Gaal akitaka kuwaondoa Welbeck, Tom Cleverly, 25, na Shinji Kagawa, 25 (Daily
Telegraph), Cleverly yuko tayari kusalia hadi mwaka ujao mkataba wake
utakapokwisha (Independent), Sunderland wametoa dau la pauni milioni 6
kumsajili beki Virgil van Dijk, 23, kutoka Celtic baada ya Toby Alderweireld,
25 wa Atletico Madrid kukataa kwenda kuichezea Black Cats (Times), mchezaji wa
zamani wa Juventus Allesandro Del Piero amekubali kujiunga na Delhi Dynamos ya
India baada ya mkataba wake na Sudney FC kumalizika (Football Italia), Crystal
Palace wanajiandaa kumsajili tena Wilfried Zaha kutoka Manchester United baada
ya Neil Warnock kurejea kama meneja (Daily Star), kiungo wa Real Madrid Xabi
Alonso, 32 anakaribia kujiunga na mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich kwa pauni
milioni 8 (Guardian), Real Madrid wanataka kumsajili Marco Reus lakini wapo
tayari kusubiri hadi msimu ujao (AS), Chelsea wamekubali euro milioni 12.5
kutoka AC Milan kumsajili Fernando Torres (The Sun), Borussia Dortmund
wameonesha nia ya kumrejesha Shinji Kagawa katika Bundesliga, baada ya
kushindwa kuwika akiwa Old Trafford (Kicker), maafisa wa Juventus wamekutana na
maafisa wa Monaco kujadili suala la Radamel Falcao kwa mkopo (Gazetta dello Sport),
Inter Milan wanataka kumchukua Xherdan Shaqiri kutoka Bayern Munich, iwapo
Ricky Alvarez ataondoka wiki hii kwenda Sunderland (Corriere dello Sport) Diego
Costa huenda akakosa kucheza kwa wiki sita baada ya kuumia msuli wa paja (Daily
Telegraph). Zimesalia siku nne kabla ya dirisha la usajili kufungwa. Tetesi
nyingine kesho tukijaaliwa. Cheers!!!
No comments:
Post a Comment