Pages

Friday, August 29, 2014

TETESI ZA SOKA ULAYA



Real Madrid wamekamilisha uhamisho wa pauni milioni 20 wa Radamel Falcao, 28, kutoka Monaco (Calciomercato), Arsenal wana matumaini ya kukamilisha uhamisho wa beki Sorkatis Papastathopoulos, 26, kutoka Borussia Dortmund, lakini wamesema hawatalipa pauni milioni 20 (Daily Mirror), boss wa Aston Villa Paul Lambert ametoa dau la pauni milioni 8 kumtaka kiungo wa Manchester United Tom Cleverly, 25, (Daily Telegraph), lakini

 Lambert huenda wakapata upinzani mkali kutoka Valencia, ambao nao pia wamepanda dau kwa Cleverly (Sky Sports), Danny Welbeck, 23, anajiandaa kuondoka Old Trafford, na akitajwa kwenda Tottenham kwa mkopo (Daily Star), Chelsea wanakaribia kutoa ruhusa kwa Fernando Torres, 30, kwenda Inter Milan (Times), Manchester United wameongeza bidii kumfuatilia kiungo Martin Odegaard, 15, anayechezea Stromsgodset kutoka Norway (Daily Telegraph), Valencia na Juventus wametoa dau la kutaka kumsajili Javier Hernandez, 26, kutoka Manchester United kwa kiasi cha pauni milioni 15 (Guardian), mshambuliaji Demba Ba, 29, alikaribia kujiunga na Arsenal kabla ya kusaini kwenda Besitkas ya Uturuki kutoka Chelsea kwa pauni milioni 8 (Independent), kiungo anayesakwa na Manchester United Arturo Vidal, 27, amekaririwa akisema hataki kuondoka Juventus (Daily Express), kiungo wa zamani wa Arsenal Alex Song, 26, ana matumaini ya kurejea katika Premier League na Liverpool baada ya Barcelona kuonekana kutomtaka (Daily Mirror), kiungo wa PSG Adrien Rabiot ambaye mkataba wake unaisha msimu ujao anasakwa na Roma na Arsenal (Le Parisien). Zimesalia siku tatu kabla ya dirisha la usajili kufungwa. Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Cheers!!

No comments:

Post a Comment