LIGI kuu soka nchini England imeanza leo kwa mechi saba kupigwa katika viwanja tofauti.
Mechi ya mapema ilishuhudiwa katika dimba la Old Trafford
ambapo wenyeji Manchester United chini ya kocha mpya, Mholanzi, Louis Van Gaal
walilala 2-1 dhidi ya Swansea City.Katika mechi nyingine za Jioni, Leicester
City wakiwa nyumbani wamelazimisha sare ya mabao 2-2 dhidi ya Everton.
QPR wakiwa nyumbani wamechapwa bao 1-0 na Hull City, wakati
Stoke City nao wamelala 1-0 wakiwa uwanja wa nyumbani dhidi ya Aston Villa.
Katika mechi nyingine West Brom wametoka sare ya mabao 2-2
na Sunderland.
Tottenham wakiwa ugenini wameshinda bao 1-0 dhidi ya wenyeji
West Ham United.
Mechi ya mwisho leo hii inaendelea baina ya Asernal dhidi ya
Crystal Palace katika uwanja wa Emirates mjini London.
Ligi hiyo itaendelea kesho ambapo washindi wa pili wa msimu
uliopita, Liverpool watakuwa katika dimba lao la Anfield kuchuana na
Sounthampton, wakati mabingwa Manchester City wataoneshana kazi ugenini na
Newcastle United.
No comments:
Post a Comment