Pages

Friday, August 22, 2014

UTAFITI: MWANAMKE HUONA BORA ABAKI SINGLE KULIKO KUWA NA MWANAUME MWENYE SIFA HIZI


1.Unampiga sana na Kukasirika kwa vitu ambavyo havina msingi. Humpi muda wa kuwa na rafiki, simu yake ni ya kwako (yaani unayajua majina yote na sms zote!)


2.Unamtumia dada/mama yako kumuonya, kumnunulia vitu, na unatumia muda mwingi na dada au mama kuliko yeye

3.Unamtegemea mwanamke  kupita kiasi, unapata huduma zote kutoka kwake, una mipango mingi na haoni ukiifanyia kazi zaidi ya ahadi zisizoisha.

4.Huwezi kutumia mikono yako (huwezi kufanya kazi ndogo ndogo kama kubadilisha taa iliyoungua, tairi la gari, Huko tayari kuchafuka na huwezi kufanya kazi ndogondogo za kiume)

5. Unakunywa pombe kupindukia na unaishia kuweka mipango ya kimaisha isiyokamilika. Na huujali mwili wako!

ENDELEA KUSOMA MAKALA HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI


6.Unamsema vibaya mbele ya watu. Na kila mara mna ugomvi usiomalizika

7.Siku zote wewe ndio wa mwisho mbele ya wanaume wenzio. Pengine wewe ni mnyonge kupitiliza, au unamuaibisha kwani kila mwanaume anaonekana ana ubora, mkakamavu, anachapa kazi kuliko wewe.

8.Kila siku huna hela na hujui utapata lini.

9.Hubadiliki! una aina moja tu ya maisha, mapenzi yenu hayana vitu vipya wala ubunifu.

10. Unamtambulisha mno kwa marafiki wa kike kuliko wa kiume (au ndugu wakiki kuliko wa kiume)

MAKALA HII IMEANDALIWA NA 10 MUHIMU

No comments:

Post a Comment