Na Mwandishi wetu
WATU watatu wamefariki dunia na wengine sita kujeruhiwa
baada ya kulipukiwa na bomu katika kijiji cha Migongo Wilaya ya Buhigwe Mkoani
Kigoma wakiwa ndani ya gari la abiria
aina ya Hiace.
Akizungumzia tukio hilo leo hii, Mwenyekiti wa Kijiji cha
Kilelema, Benedicto Mahuta, alisema kuwa
tukio hilo lilitokea mida ya saa 11 alfajiri ambapo majambazi watano ndio
walitekeleza tukio hilo wakati wakiwa kwenye jitihada za kuliteka.
Alisema kuwa awali gari hilo lilikuwa linaelekea Kasulu na
lilipofika katikati ya pori la Kasesema
walikuta mtu mmoja amesimama barabarani
akiwa na bunduki ili kusimamisha gari lakini dereva hakusimama, baada ya hatua
15 walikuta mtu mwingine amesimama baada ya kumpita kidogo ndipo bomu likapigwa
na kulipuka kwenye gari.
“Kwa mujibu wa dereva wa gari lile, baada ya bomu kulipuka hakusimama kwa kuhofia
kutekwa moja kwa moja na watu wale hivyo
wakaenda kusimama karibu na kambi ya
Jeshi la wananchi na kutoa taarifa ila tayari bomu lile lilikuwa limesha ua na
kujeruhi.
Aidha Muhita alisema kuwa Wanajeshi walipopata taarifa
walienda haraka eneo la tukio na walipofika
walikuta wale majambazi walisha kimbia
ila wakakuta mwili wa mototo ambaye baada ya bomu kulipuka alitupwa nje ya gari
na kufariki.
“Jumla ya watu
waliofariki dunia ni watatu na wengine sita kujeruhiwa, ila majeruhi
walikimbizwa katika kituo cha afya cha Muyama, pia baaba ya Jeshi la wananchi
kufika eneo la tuki na sisi kufika walitutaka kutoa ushirikiano ili kubaini
majambazi wale walikimbilia wapi” aliongeza Muhita
Nae mmoja wa abiria aliyenusulika katika tukio hilo,
Agostino Mkuvata alisema kuwa walipofika
eneo la pori walikuta mtu mmoja akiwa ameshika bunduki huku akiielekeza kwenye
gari ila kwasababu ilikuwa ni alfajiri na taa za gari zilikuwa zimewaka, dereva
alifanikiwa kumpita na walipofika mbele wakamkuta mwingine ambaye baada ya kumpita
bomu likapigwa kwenye gari.
“Mwanzo hatukujua kama ni bomu ila tulisikia kitu kimetupwa
kwenye gari ila kwasababu mimi nilikuwa nimekaa mbele nilimwambia dereva
asisimame kwa usalama zaidi, ndipo
abiria waliokuwa sehemu ya nyumba ya gari wakaanza kupiga kelele kuwa dereva
simamisha gari tunakufa” alisema Mkuvaka.
Kwa upande wa Mkuu wa Kituo cha Polisi Cha Wilaya ya
Buhigwe, Frank Utonga, alisema kuwa taarifa walishazipata na waliofariki ni
watu watatu na majeruhi sita ila hakuna mtu waliomshikilia ila upelelezi
unaendelea.
No comments:
Post a Comment