Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – SACP
Na: Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linawashikilia watu watano (5)
kwa kuhusika na mauaji ya madereva wawili wa bodaboda kwa nyakati tofauti.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi
wa Polisi DAVID MISIME – SACP amesema watuhumiwa watatu ambao ni ALEX S/O
LETEMA LEWENJE mweye umri wa miaka 20, Mkaguru, ANDREA S/O MAJUTO CHIGUNDULA mwenye
umri wa miaka 24, Mkaguru na NABAKI S/O MAUNGO MWIGOE mwnye umri wa miaka 23,
Mkaguru wote wakazi wa Gairo Mkoa wa Morogoro ambao wanashikiliwa kwa tuhuma za
kumwuua JACKSON S/O JOHN MASAUSE tarehe 01/07/2014
huko katika Kijiji cha Lenjulu, Tarafa ya Mlali Wilayani Kongwa kisha kuchimba shimo na kumfukia na kupora pikipiki yenye namba za usajili T. 374 CXH aina ya FEKON pamoja na simu yake.
huko katika Kijiji cha Lenjulu, Tarafa ya Mlali Wilayani Kongwa kisha kuchimba shimo na kumfukia na kupora pikipiki yenye namba za usajili T. 374 CXH aina ya FEKON pamoja na simu yake.
Pia Kamanda
MISIME amesema watuhumiwa hawa baada ya kukamatwa walikiri ni kweli walimkodi
marehemu tarehe 01/07/2014 na wakaenda kuonyesha walikoficha pikipiki hiyo na
simu huko Gairo. Mwili wa marehemu uligundulika tarehe 01/08/2014 na shoka
walilotumia kumpiganalo kichwani lilikutwa pembeni ya sehemu walipo mfukia
marehemu.
Kamanda
MISIME ameongeza kuwa watuhumiwa wengine ni ALLY S/O NURDIN ITEKULE mwenye umri
wa miaka 25, Mrangi pamoja na HALIFA S/O JUMA MSALA mwenye umri wa miaka 28,
Mrangi wote wakazi wa Swaswa Dodoma Mjini na Kondoa ambao wanatuhumiwa
kumkodisha dereva wa bodaboda MARTIN S/O VICTORY MKORO mwenye umri wa miaka 22,
Msandawe Mkazi wa Njedengwa tarehe 26/07/2014, kisha kumuua kwa kumkata na kitu
chenye ncha kali shingoni na kumjeruhi sehemu mbalimbali za mwili kisha kupora
pikipiki yenye namba za usajili T. 777 CPR ambayo ilipatikana baadaye. Tukio hilo
walilifanya katika eneo la Njedengwa karibu na makaburi ya Chaduru.
Watuhumiwa walikamatwa
wakiwa huko Kidoka katika Wilaya ya Chemba wakiuza pikipiki nyingine yenye
namba za usajili T. 372 CHF aina ya Boxer wailiyoipora tarehe 27/07/2014 na walikiri
kumuua MARTIN S/O VICTORY MKORO pia walifanya hivyo kwa sababu alikuwa
anawafahamu ili asije akawasema lakini wakasahau kuwa mkono wa dola ni mrefu. Watuhumiwa
hawa wanahojiwa pia kwa matukio mengine ambayo wamekiri kuhusika na uchunguzi
ukikamilika watafikishwa mahakamani.
Aidaha Kamanda
MISIME amesema mtandao huu wa watuhumiwa hawa umegundulika kutokana na
ushirikiano mzuri wa wananchi. Polisi Mkoa wa Dodoma wanawashukuru sana
wananchi kwa ushirikiano huo.
Kamanda MISIME
ametoa wito pia kwa wahalifu kuwa uhalifu haulipi hivyo wabadilike na kuwa
wananchi wema wanaochukia uhalifu.
No comments:
Post a Comment