Jeshi la Lesotho
Waziri mkuu nchini Lesotho Tom Thabane ameiambia BBC kwamba
amelitoroka taifa hilo baada ya kupata vitisho vya maisha yake.Akizungumza
kutoka nchini Afrika kusini,Bwana Thabane amesema kuwa vitenmdo vya jeshi
nchini humo vimesitisha huduma za serikali na kusababisha mapinduzi.
Awali Ripoti kutoka mji mkuu wa maseru zilizsema kuwa jeshi
lilizingira makao makuu ya polisi na kuzuia matangazo ya radio pamoja na mtandao
wa simu katika mji mkuu wa Maseru.
Uchaguzi uliozongwa na utata nchini humo miaka miwili
iliopita ulisababisha kuundwa kwa serikali ya muungano isio dhabiti.
Licha ya mazungumzo ya kuleta amani mnamo mwezi Juni ,hali
ya wasiwasi ilitanda huku majirani wa taifa hiilo wakionya dhidi ya mbinu
yoyote isio ya kikatiba.
Taifa hilo limezungukwa na Afrika kusini na hutegemea sana
jirani yake kwa masli asli pamoja na nafasi za kazi.
(E.L)
No comments:
Post a Comment