Mkurugenzi wa shirika la afya duniani Margeret Chan amesema kuwa kuzuka kwa ugonjwa wa Ebola Magharibi mwa Afrika kunaweza kusababisha janga baya iwapo hautazuiwa.
Akizungumza mjini Conakry baada ya kukutana na marais wa Guinea,Liberia na Sierra Leone,amesema kuwa ugonjwa huo unasambaa kwa kasi ikilinganishwa na juhudi za kuudhibiti,lakini akaongezea kuwa unaweza kusitishwa kutokana na usaidizi wa kimataifa.
Marekani imesema kuwa raia wawili wa taifa hilo wa kutoa msaada wanaougua ugonjwa wa ebola watasafirishwa hadi nchini Marekani mapema wiki ijayo ili kupewa matibabu katika eneo lililotengwa.
Kisa hicho cha ugonjwa huo kitakuwa cha kwanza kutibiwa marekani.Chanzo BBC Swahili
No comments:
Post a Comment