Pages

Wednesday, August 27, 2014

ZITAMBUE TABIA MBAYA ZA KIUONGOZI AMBAZO ZINAHARIBU MAKAMPUNI

Nimesikia msemo unaosema watu huwa hawayaachi makampuni bali huwaacha mameneja au huwakimbia mameneja wa makampuni hayo. Kam hivyo ni kweli, kuna baadhi ya mameneja wanaweza kuwaweka watu ndani au kuwataabisha wafanyakazi wao. Je tabia gani mbaya ambazo zinakimbiza vipaji kwenye makampuni?


Kama uko kwenye nafasi ya uongozi sasa huu ni wakati wa kutilia maanani hili mambo. Hapa kuna baadhi ya tabia ambazo unatakiwa uondokane nazo kama unataka ubakie na vipaji kwenye kampuni au shirika unaloliongoza ili liweze kufanikiwa.

1. Kushindwa kuwasikiliza unaowaongoza

Je wewe huwasikiliza watu unaowaongoza wakileta wazo fulani kwako? Je unasikiliza mawazo yao wakati wa vikao?Je unajali wanachokiongea? Kwasababu unafanya kazi na watu wa tabia na hulka mbalimbali, inakupasa utilie maanani kila mambo ambalo linaletwa kwkao na kulifanyia kazi ipasavyo ili kuweza kusuluhisha na kupambana na changamoto kwenye kundi unaloliongoza. Kiongozi mzuri anajua kitu gani watu wake wanafanya, huchukua muda kuwasikiliza na wanapohitaji msaada huwa karibu yao kuwasaidia. Kushindwa kuwasikiliza kunasababisha msongo wa mawazo kwa watu unaowaongoza na watu hao hukosa tumaini juu ya viongozi wao kwenye kampuni au mashirika.

2. Kushindwa kutumia vipaji ulivyonavyo kwenye kundi unaloliongoza

Kila timu ina watu wenye vipaji tofauti tofauti , vipaji hivyo vinaweza muleta matokeo mazuri kwenye kampuni na shirika kwa ujumla. Je wewe unajua vipaji ulivyonavyo kwenye timu yako? Je umepata muda wa kuongea na kila mtu kujua namna ya kuweza kumsaidia kutumia kipaji chake au ujuzi wake ipasavyo? Je umeweza kuongea na kila mtu kujua uwezo alionao katika taaluma yenu kwenye biashara au shughuli mnazozifanya? Kama umeshindwa kufanya hivyo unafanya kazi gizani sana.
Kiongozi mzuri huhusisha watu wake na kutumia ujuzi na vipaji vyao kuleta matokeo bora kwenye taasisi anayoiongoza. Kushindwa kufanya hivyo, huleta kukata tamaa kwa wafanyakazi, kukosa motisha na kuzorota kiutendaji kazi.

ENDELEA KUSOMA MAKALA HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI



3. Kushindwa kutambua kazi za watu unaowaongoza
Je ni lini uliwapongeza watu unaowaongoza? Je huwa unatambua juhudi zao kwa kusema mafanikio na kumtambua kila mmoja anayefanya vyema kwenye kampuni yenu? Kiongozi mzuri huchukua muda vile vile kutambua na kuwapongeza wanaofanya vizuri kila wakati inapotokeo hivyo. Kushindwa kufanya hivyo kunahatarisha kampuni na maendeleo yake.

4. Kuficha Habari kwa unaowaoongoza

Je unafanya nini kuhakikisha wanapata habari ya kila kinachoendelea? Je unatoa mrejesho chanya na hasi pia kwa watu unaowaongoza? Je kama kuna tatizo kwa mmojawapo kwenye kundi unashughulika nalo kivipi? Je unakusanya ushahidi wowote kabla ya kufanya maaamuzi au unakurupukia kufanya maamuzi kabla ya kukusanya ushahidi wa kutosha? Kiongozi mzuri ni mwaminifu kwa watu anaowaongoza kwa kuwapa habari kwa usahihi na kurekebisha panapostahili, hapo inapohusisha wafanyakazi hao. Kushindwa kuwasiliana vizuri na timu yako kuna madhara kiutendaji na mafanikio yenu.

5. Je unatoa majibu?

Je huwa unajibu swali au unapindisha majibu ya swali pale wafanyakazi wanapohitaji majibu? kama hauko tayari kutoa majibu ya msingi kwa wale unaowaongoza, nao wanakata mawasiliano na wewe kwa kuwa huna msaada kwao.

6. Kuwa mtemi

Je wewe ni mtemi katika maamuzi, mawazo na utendaji? Je wewe unazuia watu unaowaongoza kuwafikia viongozi wa juu? Kama wewe ni mtemi unayefanya watu wakuogope, haitakusaidia kufanya vyema kwenye kiting chako.

7. Kuwa na visasi au hasira
Inawezekana mmoja wa wale unaowaongoza hajakubaliana na wazo lako au kile ulichowasilisha au hata maamuzi uliyofanya. Je unachukua hayo maamuzi kwa hasira au kutafuta namna ya kumkomesha? Kama unafanya hivyo wewe hiyo sio tabia nzuri hasa kama wewe ni kiongozi. Kiongozi mzuri anakubali rejea kutoka kwa watu anaowaongoza inapokua nzuri au mbaya. Kampuni inaongozwa vyema pale kila mmoja anapowajibika ipasavyo, pale unapozuia watu unaowaongoza kutoa sauti zao hawakuamini wala kukuthamini kama kiongozi wao.

8. Unyanyasaji au matumizi ya nguvu kihisia

Inawezeka huwapigi kwa ngumi bali namna gani unatumia nafasi yako kama kiongozi wao? Je kihisia unawafanyia nini wafanyakazi wake? Je unawaheshimu wafanyakazi wako? Kama kiongozi unatakiwa kuwaheshimu wafanyakazi wake au watu unaowaongoza kihisia, kitaaluma na hata muonekano wao, hivyo unatakiwa kutofautisha mambo ya kikazi na binafsi kwao ili kuboresha mahusiano nao.
Je wewe huwa unafanya mini? Unachotakiwa kujua kila unachokifanya huharibu kampuni au taasisi taratibu bila ya wewe kujua. Siku moja utakuta kampuni yako haipo tena au taasisi inapata shida kiutendaji na unatafuta mtu wa kumlaumu. Una nguvu ya kuhakikisha kampuni au taasisi inakwenda juu au chino kila kitu kilo mikononi mwako.

No comments:

Post a Comment