Pages

Saturday, September 13, 2014

AFISA UVUVI IRINGA AFA KATIKA AJALI YA PIKIPIKI NA CANTER IRINGA



Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Wiliamu Mwanzoka mwenye umri wa miaka 30 ambaye alikuwa ni afisa uvuvi halimashauri ya wilaya ya kilolo Mkoani Iringa amefariki akiwa anaendelea na matibabu katika hospitari ya Mkoa Iringa baada ya kugongwa na gari no:T 789BMF aina ya mitshubish Canter iliyokuwa ikiendeshwa na Ordo Leornad mkazi wa eneo la Mtwivila Manispaa ya Iringa.



Aidha amesema ajali hiyo imetokea kijiji cha Kilolo barabara ya Kilolo-Iringa wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa na marehemu amegongwa akiwa anaendesha pikipiki no: STL 483 aina ya Honda mali ya halmashauri ya Wilaya ya Kilolo Mkoa wa Iringa ambapo chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi na dereva wa gari hilo anaendelea kushikiliwa na jeshi la polisi kwa uchunguzi zaidi.

No comments:

Post a Comment