Askari watakiwa kutoa huduma bora kwa jamii
Na Frank Geofray – Jeshi la Polisi, Moshi.
Askari kote nchini wametakiwa kuendelea kutoa huduma bora kwa jamii, kwa kuwa kufanya hivyo kutasaidia kuimarisha na kuboresha uhusiano mwema na jamii ambao utasaidia kukabiliana na vitendo vya uhalifu na wahalifu vinavyojitokeza hapa nchini.
Hayo yalisemwa jana na Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi Nchini, Abdulrahman Kaniki wakati alipokuwa akifungua mkutano wa Maafisa
wanadhimu, wahasibu na watunza stoo kutoka mikoa na vikosi vya Jeshi la Polisi kote nchi ni unaoendelea mkoani Kilimanjaro katika chuo cha Polisi Moshi (CCP) ukiwa na kauli mbiu isemayo usimamizi wa raslimali ni tunu ya Jeshi la Polisi kwa maendeleo yake
Kaniki alisema askari wote wanapaswa kutoa huduma bora kwakuwa wananchi ndio wanaotoa tathmini ya huduma zinazotolewa na jeshi hilo hivyo wananchi watakapopata huduma bora wataendelea kutoa taarifa ambazo zitasaidia kuwabaini wahalifu wanaoishi nao katika jamii inayowazunguka.Na Frank Geofray – Jeshi la Polisi, Moshi.
Askari kote nchini wametakiwa kuendelea kutoa huduma bora kwa jamii, kwa kuwa kufanya hivyo kutasaidia kuimarisha na kuboresha uhusiano mwema na jamii ambao utasaidia kukabiliana na vitendo vya uhalifu na wahalifu vinavyojitokeza hapa nchini.
Hayo yalisemwa jana na Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi Nchini, Abdulrahman Kaniki wakati alipokuwa akifungua mkutano wa Maafisa
wanadhimu, wahasibu na watunza stoo kutoka mikoa na vikosi vya Jeshi la Polisi kote nchi ni unaoendelea mkoani Kilimanjaro katika chuo cha Polisi Moshi (CCP) ukiwa na kauli mbiu isemayo usimamizi wa raslimali ni tunu ya Jeshi la Polisi kwa maendeleo yake
Pia amewataka washiriki wa mkutano kutumia fursa waliyoipata katika kuweka mipango ya pamoja itakayosaidia kupunguza uhalifu na kuhimarisha amani na utulivu unaoendelea hapa nchini ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa bajeti ya jeshi la Polisi.
Aidha amewapongeza askari kwa utendaji wao wa kazi ambao umesaidia nchi kuwa katika hali ya amani na utulivu licha ya kukumbana na changamoto mbalimbali katika utendaji kazi wao wa kila siku.
Kwa upande wake Kamishna wa fedha na logistiki Clodwig Mtweve, alisema lengo la mkutano huo ni kutathmini hali ya utendaji wa Jeshi la polisi na kutafutia ufumbuzi changamoto zinazolikabili hasa katika upande wa rasilimali.
“Kupitia mkutano huu utaboresha mipango yetu katika matumizi ya raslimali tulizonazo na kuhakikisha zinaleta tija kama ilivyokusudiwa jambo ambalo ni muhimu katika maendeleo ya Jeshi letu la Polisi.”Alisema Mtweve.
No comments:
Post a Comment