Kundi la Boko haram limefanya mashambulizi katika mji wa
Bama na kusababisha mauaji ya watu wengi huku wengine wakitoroka.
Wanamgambo hao waliuteka mji wa Bama ,ambao ni wa pili kwa
ukubwa katika jimbo la Borno siku ya Jumatatu baada ya jaribio la awali la
kutaka kuuteka mji huo kuzimwa na vikosi vya serikali.
Akizungumza na BBC ,wakaazi wamethibitisha kuwa mji huo
umetekwa na kundi hilo na kwamba maelfu ya watu sasa wameachwa bila makao.
Mamlaka ya Nigeria bado haijatoa tamko lolote kuhusu
shambulizi hilo.
Taarifa zinasema kuwa watu wengi wametoroka wakiwemo
wanajeshi.
Hapo awali jeshi la Nigeria lilitoa ripoti kuonyesha kuwa mpaka sasa limewaua wapiganaji 70 wa Boko Haram ,kutokana na mapigano kati ya kikundi hicho na wanajeshi Kaskazini -Mashariki mwa mji wa Bama.
Boko Haram walifika mapema asubuhi katika mji huo kwa magari
ya kivita.Taarifa kutoka katika mji huo zinaeleza kwamba mashambulizi
yalianzishwa na vikosi vya jeshi la Nigeria.
Msemaji wa kundi hilo la Boko Haram ameelezea hali ya mji
huo kwa sasa kuwa wakaazi wa mji wa Bama wamekimbilia katika mji mwingine wa
Borno na Maiduguri .
Nalo shirika la Amnesty International limetoa takwimu kuwa
raia wapatao milioni nne wamekufa mwaka huu katika mgogoro huo kati ya Boko
Haram na vikosi vya ulinzi vya Nigeria.
Wanajeshi wa serikali ya Nigeria.
No comments:
Post a Comment