wakati serikali ikiendelea kupiga vita waganga wa kienyeji
matapeli hali imekuwa tofauti huko Geita ambapo diwani wa CCM Mawazo Wiliam
wa kata ya ya Bugarama Wilayani
Geita amekamatwa akiwa na matunguri anayoyatumia nyumbani kwake kupiga ramli
chonganishi na kuosha wakataji wa mapanga .
Wakiongea kwa nyakati tofauti jana baadhi ya wananchi wa
kata hiyo kwa sharti la kutotaka
kutajwa majina yao walisema diwani huyo amekuwa ni kero kwa watu
kwani amekuwa akiwatapeli watu kwa kuwapatia tiba za uongo na kuwachonganisha
watu bila kuona kuwa yeye ni kiongozi.
Walisema diwani huyo amekuwa akiwapigia ramli chonganishi
watu wanaokwenda kwake kwa ajili ya kupata tiba ya kienyeji hivyo kuwaomba
wanaohusika kuchukua hatua dhidi ya diwani huyo.
"Jamani huyu diwani wa CCM ni tapeli anawachonganisha
wananchi mpaka wanafika hatua ya kuuana ,kwanza si mganga bali ni tapeli ni
mganga gani ufike unaambiwa kiasi kikubwa cha fedha ",walisema.
Afisa mtendaji wa kata hiyo Juma Choba alikiri kukamatwa kwa diwani wake lakini akasema kuwa alikamatwa kwa tuhuma za kuwaosha wakataji wa
mapanga katika kata hiyo.
Hata hivyo alisema hajui kama ni kweli anafanya kazi hiyo
kwani hajawahi kuona ila anasikia kutoka kwa wananchi kuwa diwani wake
anawapigia ramli chonganishi.
"Mimi nasikia kama wewe unavyosikia lakini sijawai
kumuona ila amekamatwa yuko Polisi Wilayani inawezekana ni kweli kwa kweli
siwezi kukataa",alisema Mtendaji huyo.
Akizungumza na malunde1 blog iliyotaka kujua zaidi kuhusu
tuhuma hizo za kukamatwa kwake na kupiga ramli chonganishi , diwani Mawazo
alisema kuwa yeye hana lolote la kujibu juu ya hilo.
Jeshi la polisi
Mkoani Geita limethibitisha kukamatwa kwa diwani Mawazo na uchunguzi
unaendelea kubaini ukweli wa tukio hilo.
Na Valence Robert-Malunde1 blog-Geita
No comments:
Post a Comment