Rais wa Marekani Barrack Obama hii leo anatazamiwa kutangaza
mpango wake wa kuwatuma wanajeshi 3,000 nchini Liberia kama njia moja ya
kusaidia katika vita dhidi ya ugonjwa hatari wa Ebola.
Wanajeshi hao watasimamia ujenzi wa vituo vipya vya
kimatibabu na pia watahusika katika utoaji wa mafunzo ya kimatibabu kwa
wahudumu.
Kumekuwa na malalamishi kwamba jamii ya kimataifa imelegea
katika harakati za kukabiliana na mkurupuko wa Ebole katika mataifa ya Afrika
magharibi.
Wanajeshi hao watatumika kuunda muundo msingi wa kupamabana
na Ebola Liberia
Mataifa ya Sierra Leone, Liberia na Guinea ndiyo
yaliyoathirika zaidi huku zaidi ya watu 2,400 wakiwa tayari wamepoteza maisha
yao kufikia sasa.
Zaidi ya nusu ya idadi ya watu waliofariki kutokana na
ugonjwa huu ni raia wa Liberia.
Shirika la afya duniani (WHO) limetahadharisha kuwa huenda
watu zaidi wakazidi kufariki.
Umoja wa Mataifa (UN) unapangiwa kuzungumzia jinsi ya
kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola katika mkutano unaopangiwa kufanyika
huko Geneva.
Kulingana na viongozi nchini Marekani, mpango wao wa
kukabiliana na ugonjwa wa Ebola unalenga-:
Zaidi watu 2400 wameaga dunia kutokana na Ebola
Utoaji wa mafunzo ya kimatibabu kwa wahudumu wa kiafya 500
kila juma.
Ujenzi wa vituo vya matibabu 17, kila chumba kikiwa na
vitanda kumi.
Usambazaji wa vifaa vya huduma ya afya kwa kila
nyumbaKampeni ya kuwahamasisha wananchi kuhusu jinsi ya kuwashughulikia
wagonjwa wa Ebola.
Ujenzi wa kituo cha kijeshi cha pamoja mjini Monrovia
kitakachotumiwa katika shughuli ya kupokea msaada kutoka kwa jamii ya
kimataifa.
Wadadisi wa masuala ya kimatibabu wamepongeza mpango huu wa
Marekani huku wengine wakitilia shaka nia ya Marekani nchini Liberia.
No comments:
Post a Comment