Msiba! Bado bundi wa vifo anaendelea kung’ang’ania tasnia ya
sinema za Kibongo kufuatia kifo cha ghafla cha msanii wa Bongo Muvi, Mariam
Juma ‘MC Chimamy’ ambaye amefariki dunia ghafla baada ya kupatwa na kifafa cha
mimba, ugonjwa uliomkuta
muda mfupi kabla ya kujifungua.
Msanii wa Bongo Muvi, Mariam Juma ‘MC Chimamy’ enzi za uhai
wake.
Mauti hayo yalimkuta MC Chimamy wikiendi iliyopita baada ya
kukimbizwa kwenye Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar, akiwa tayari na hali
mbaya kwani kabla ya hapo alianzia Hospitali ya Palestina, Sinza ambapo
alilazimika kukimbizwa katika hospitali hiyo ya Wilaya ya Kinondoni ili
kunusuru maisha yake na kiumbe alichokuwa nacho tumboni.
Msiba huo umezua simanzi kubwa kwa wasanii wenzake hasa
Vanita Omary, Halima Yahya ‘Davina’, Yvonne-Chery Ngatwika ‘Monalisa’, Mariam
Kakwaya na wengine kwani alikuwa ni mtu wao wa karibu na siku aliyokutwa na
umauti alikuwa amepangwa kuwa mshereheshaji wa shughuli ya Davina ya kibao kata
iliyofanyika Bamaga-Mwenge, Dar.
“Msiba huu umenishtua sana, sikutarajia kama Chimamy
angetutoka kimchezo hivi, ukweli nimeumia sana na sina la kusema, namshukuru
Mungu kwa kazi yake,” alisema Vanitha
No comments:
Post a Comment