Maiti nyingi bado zimefukiwa katika kifusi hiki na jitihada
za uokoaji zinaendelea.
Idadi ya watu waliokufa kwenye Kanisa la Synagogue of All
Nations (SCOAN) la Nabii TB Joshua nchini Nigeria inatisha baada ya Rais wa
Afrika Kusini, Jacob Zuma, kusema raia 67 wa nchi nao wamepoteza maisha.
kwamba
vifo vya raia hao wa Afrika Kusini vimethibitishwa rasmi na ubalozi wa Afrika
Kusini nchini Nigeria.
Mamia ya watu waliojeruhiwa vibaya baada ya kanisa hilo
kuporomoka Ijumaa iliyopita.
“Huu ni wakati mgumu sana kwa Afrika Kusini. Katika historia
ya karibuni ya nchi hii hatujawahi kuwa na idadi kubwa kama hii ya vifo vya
mara moja nje ya nchi yetu," alisema Rais Zuma.
“Tunazihuzunikia familia, marafiki na jamaa za waliopoteza
maisha.
“Taifa zima linaungana nao katika majonzi ya mama, baba.
mabinti na vijana waliopoteza wapendwa wao. Sote tupo katika maombolezo,”
alisema.
Jumanne jioni, Clayson Monyela, msemaji wa Idara ya Uhusiano
wa Kimataifa aliandika kwenye akaunti yake ya tweeter kwamba serikali ilikuwa
inahangaika kupata taarifa za janga hilo.
Zuma alisema alikuwa ameziagiza idara mbalimbali za serikali
kuhakikisha kwamba ndugu wa marehemu hao wanapelekwa Nigeria kutambua miili ya
ndugu zao na kwamba serikali imeagiza miili hiyo irejeshwe haraka nyumbani
Afrika Kusini.
Taarifa hizo zimekuja kwa mshtuko kwamba yawezekana
waliokufa ni zaidi ya 100 kwani jengo hilo la kanisa, ambalo lina nyumba ya
kulala wageni, lilikuwa na watu wengi kutoka mataifa mbalimbali wakati
linaporomoka.
No comments:
Post a Comment