Baadhi ya Kamati za Bunge Maalum la Katiba zimependekezwa kuwepo kwa Ibara mpya inayohusu kuanzishwa kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa na Uhujumu Uchumi katika sura ya 15 ya Rasimu ya Katiba inayopendekezwa.
Hayo yamebainika leo wakati wa uwasilishaji wa taarifa za Kamati Namba Moja hadi Kamati Namba Kumi na Mbili za Bunge hilo kuhusu uhakiki wa Rasimu hiyo uliofanyika kwenye kikao cha arobaini na tatu kilichofanyika mjini Dodoma.
Taarifa hizo,ambazo zimewasilishwa na baadhi ya wenyeviti wa Kamati hizo na baadhi ya wajumbe kutoka 201 waliopewa ridhaa za kuwasilisha.
Akizungumzia kuhusu suala hilo Makamu Mwenyekiti wa Kamati Namba Mbili, Shamsa Mwangunga alisema katika Kamati yake baada ya kupitia na kujadiliana suala la kuongeza ibara inayohusiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa na Uhujumu Uchumi.
“ Katika sura ya 15 ninayohusu Taasisi za Uwajibikaji, Kamati inapendekeza kuwe na Ibara inayoanzisha Taasisi hiyo na mambo mengine ya utafiti, uchunguzi na n.k( nakadhalika) yawekwe kwenye sheria husika,” alisema Mwangunga.
Akisoma taarifa ya Kamati Namba Sita ya Bunge Maalum la Katiba, mjumbe wa Bunge hilo, Charles Mwaijage alisema katika kukabiliana na tatizo la rushwa na uhujumu uchumi, Bunge litatunga sheria juu ya kuwepo kwa taasisi hiyo, ambapo itaainisha majukumu ya msingi ya taasisi hiyo katika utafiti, uchunguzi wa makosa kuchukua hatua stahili dhidi ya watuhumiwa na kuwafikisha mahakamani.
Mm binafsi nimeanza kuwa na wasiwasi na mzee Warioba.Anasiri gani na rasimu yake ya Katiba aliowasirisha kwa Mh. raisi.Isije ikawa ina maslahi binafsi na baadhi ya viongozi hapa nchini.Maana chapuo limepindukia sana.Maana yeye ameshakabidhi maoni ya wananchi inakuwaje anataka kuonyesha kama vile kuna baadhi ya mawazo yake binafsi anataka yapitishwe.Jambo ambalo analipigia debe hajui kuwa anaweza kusababisha mgogoro mkubwa ndani ya jamii inayomsikiliza.Kwa nini anakosa busara na hekima anataka kuwa chanzo cha kutibua amani ya nchi yetu.Yapo mambo anaweza kusimama mbele ya kadamnasi akayaongea na busara inabidi itumike.Mbona kipindi akiwa na Baba wa taifa hakushupaa hivi aliogopa nini,na kama aliogopa kipindi kile sasa ujasiri huo ameutoa wapi.Watanzania tuwe makini na wazee wa aina hii.
ReplyDelete