Pages

Thursday, September 11, 2014

KAMPUNI YA SMART CODES TANZANIA YAZINDUA HUDUMA MPYA “PATIKANA” KUSAIDIA BIASHARA ZA KITANZANIA KUONEKANA POPOTE DUNIANI‏


Kampuni ya SMART CODES inayojishughulisha na teknolojia ya mtandao, imezindua huduma mpya na ya bei nafuu kuwawezesha wafanyabiashara wote duniani hususani Tanzania kuweza kuweka bishara zao kwenye mtandao (Website).

 
Huduma hiyo itawezesha wafanyabiashara wakubwa na wale wadogo kusajili maji na ya biashara zao kwenye kikoa cha Tanzania DotTZ (.tz) mfano www.jinalabiasharayako.co.tz napia kukupa emails nyingi utakavyokupitia jina la biashara yako. Mifano ya email unazoweza kupata ni kama vile wewe@jinalabiasharayako.co.tz ambazo zitakuwezesha kufanya biashara kisasa zaidi. Pia kupitia huduma hiyo ya Patikana utapata Tovuti/Website ya kuanzia BURE kabisa.
Akitoa taarifa hizo Mkurugenzi Mkuu wa SMART CODES bwana Edwin Bruno, amesema “Kwa sasa wafanyabiashara wengi wamekua wakipoteza wateja wengi wanaowatafuta mtandao nikutokana na kutokua na Website zinazo onyesha huduma wanazozitoa, hapo ndipo tulipoona ni vizuri kuwapa watanzania wote huduma hii kwa bei sawa na bure ya TSH. 199,000 Tu! Ambapo atapata Domain Name, Hosting , Emails na Tovuti ya kuanzia”
Ili kuweza kufurahia huduma hii tembelea tovuti ya PATIKANA sasa hapa www.patikana.co.tz na ufuate maelekezo ya jinsi ya kujisajili.
Pia unaweza kuangalia video iliyopo kwenye mtandao wa huduma za PATIKANA hapa

Kwa maelezo zaidi wapigie simu kupitia 0658511115 au watumie barua pepe; support@patikana.co.tz

No comments:

Post a Comment