Bw. Ali anayedaiwa kuunganisha visivyo halali, mitambo ya
kurusha matangazo ya televisheni ya vituo mbalimbali kwa malipo rahisi.
Katika hali ya kushangaza, mtu mmoja anayefahamika kwa jina
la Ali, mkazi wa Mwananyamala jijini Dar, amekamatwa na polisi baada ya kudaiwa
kuunganisha visivyo halali, mitambo ambayo iliwawezesha watu kuangalia
matangazo ya televisheni ya vituo mbalimbali kwa malipo rahisi.
Awali, msamaria mwema mmoja alipiga simu kwa kikosi kazi cha Operesheni Fichua Maovu (OFM) cha Global Publishers na kukitonya juu ya uwezo wa mtu huyo anayewashangaza kwa utaalamu wake wa kuunganisha mitambo hiyo bila kugundulika.
No comments:
Post a Comment