Wachezaji wa Liverpool wakisherehekea ushindi
Kocha wa timu ya Liverpool Brendan Rogers amepata furaha
nyingine baada ya timu yake kuifunga Tottenham Hotspur kwa mabao 3-0.
Katika mchezo huo uliochezwa kwenye uwanja wa White Hart
Lane, mchezaji mpya wa timu hiyo Mario Balotelli, ameshindwa kuonesha cheche
zake katika mechi ambayo ilikuwa ya kwanza kwake tokea ajiunge na timu hiyo
baada ya kupoteza nafasi kadhaa za wazi.
Goli la penalti la kiungo Steven Gerrad na mawili kutoka kwa
Alberto Moreno yalitosha kuizamisha timu ya Spurs katika mchezo huo.
Liverpool walimpoteza mchezaji wao mwenye uwezo wa hali ya
juu wa kupachika mabao Luis Suarrez ambaye ametimkia huko Hispania katika club
ya Barcelona.
Katika msimu uliopita Suarrez aliifunga Spurs katika michezo
yote miwili waliokutana.
Rodgers anaendelea kuwaunganisha wachezaji wake aliowasajili
katika msimu wa kiangazi na kuweza kuibuka kidedea katika mchezo wake wa
ufunguzi dhidi ya Southarmpton kabla ya kuambulia kipigo kutoka kwa mabingwa
watetezi Manchester City jumatatu iliyopita.
No comments:
Post a Comment