picha na maktaba |
.katiba ya zamani kufanyiwa marekebisho
.Ni kuruhusu tume huru na mgombea binafsi
.Ni makubaliano ya viongozi wa vyama vya siasa
Na Lukwangule Blog
KATIBA inayotumika sasa ya mwaka 1977 itafanyiwa marekebisho
muhimu kupisha uchaguzi mkuu ujao, na Rais ajaye ataamua hatima ya katiba mpya
ya Tanzania.
Hayo yametamkwa leo na Mwenyekiti wa TCD, John Cheyo
akizungumza na waandishi wa habari .
Kwa matamko ya Cheyo mchakato wa kuandika katiba
umesitishwa.
Cheyo amesema kwamba hayo ni maamuzi yaliyofikiwa na
viongozi wa vyama vya siasa vyenye wabunge na Rais Jakaya Kikwete.
Mambo ambayo vyama vya siasa wamekubaliana ni kuwa na tume
huru ya uchaguzi na kusimamia uchaguzi wa mwaka 2015, mshindi wa uchaguzi wa
Rais ashinde kwa zaidi ya asilimia, matokeo ya uchaguzi wa rais yaweze kupingwa
mahakamani na kuruhusu mgombea binafsi katika uchaguzi.
Pia vyama vingine vya siasa ambavyo vinapenda kupendekeza
mambo mengine ya kurekebisha katika katiba ya mwaka 1977 vinaombwa kufanya
hivyo mapema kwa kuwa muda uliopo wa kufanya mabadiliko ni mdogo.
“Muda tulio nao ni kwa mabadiliko yanayopendekezwa
kujadiliwa katika Bunge la Novemba na
wakichelewa Bunge la Februari 2015,” alisema Cheyo.
Kwa makubaliano hayo, kazi inayofanywa na Bunge maalum la
katiba (BMK) ya kuandika katiba mpya
itakoma Oktoba 4 mwaka huu, siku ambayo
Bunge hilo litakuwa halijakamilisha uandikaji wa katiba ambao unafanywa na
kamati ya uandishi iliyo chini ya Andrew Chenge.
Uamuzi huo unakidhi baadhi ya madai ya kundi linalojiita
umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) ambao ni wajumbe waliokuwa ndani ya Bunge
maalum la katiba lakini walijiondoa kwa kutoridhishwa na mwenendo wa bunge
hilo.
Miongoni mwa madai yao waliyokuwa wanayataka ya kusitisha
Bunge hilo hayakufanikiwa kwani litaenda hadi mwisho.
No comments:
Post a Comment