Marekani imeanzisha mfululizo wa mashambulizi mapya ya anga
huko Syria kwa ushirikiano na nchi tano za Kiaraab zinazounga mkono mapambano
dhidi kundi la IS.
Kamanda wa Marekani anasema tayari wamefanikiwa kuangamiza
kituo cha mafunzo cha wapiganaji wa dola ya Kiislam,vifaa na magari yao huko
kaskazini na Mashariki mwa Syria.
Taarifa zinasema kuwa mashambulizi hayo yanalenga mji wa
Raqqa ambako ni makao makuu ya wapiganaji hao.
Uingereza imesema kuwa baadhi ya wapiganaji wa kundi hilo
wameuawa. Hata hivyo mashambulizi yamelenga mtandao wa Al Qaeda ambao unadaiwa
kushirikiana na wapiganaji wa kundi la kiislam ambalo limekuwa likiwalenga raia
wa Mgahribi.
No comments:
Post a Comment