Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, September 28, 2014

MATOKEO YOTE YA LIGI KUU TANZANIA 2014/2015 HAYA HAPA

Golikipa wa Polisi Morogoro, Abdul Ibad akijaribu kuokoa bila mafanikio kiki iliyopigwa na mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo September 27,2014. 

Timu ya soka ya Simba SC imelazimishwa sare ya pili mfululizo katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya jioni hii Septemba 27,2014,kufungana bao 1-1 na Polisi Morogoro Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
Hiyo ni sare ya pili mfululizo kwa kocha Mzambia, Patrick Phiri baada ya wiki iliyopita kutoka 2-2 na Coastal Union Uwanja wa Taifa, licha ya kuongoza 2-0 hadi mapumziko. 


Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi akishangilia bao aliloifungia timu yake wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara dhidi ya Polisi ya Morogoro uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Ramadhani Singano 'Messi' 

Hadi mapumziko, tayari Simba SC ilikuwa inaongoza kwa bao 1-0 lililofungwa na Mganda, Emmanuel Okwi dakika ya 32 akimalizia pasi fupi ya Mohammed Hussein ‘Tshabalala’. 

Timu ya Polisi inayofundishwa na Mohammed ‘Adoph’ Rishard ilibadilika na kuanza kusukuma mashambulizi langoni mwa Simba SC ambapo Danny Mrwanda, mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, aliisawazishia Polisi baada ya kumzidi mbio na maarifa beki Joseph Owino kabla ya kumchambua vizuri kipa Hussein Sharrif ‘Cassilas’. 

Azam FC imepata ushindi wake wa pili baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ruvu Shooting leo kwenye Uwanja wa Chamazi. 

Azam FC ambao walianza ligi kwa kuitwanga Polisi Moro kwa mabao 3-1, imeshinda mabao hayo mawili leo, yote yakitupiwa kimiani na Mrundi, Didier Kavumbagu ambaye sasa ana mabao manne. 

Matokeo mengine ya Ligi Kuu Vodacom 2014/2015 ni kama ifuatavyo:- 
Azam FC 2 - 0 Ruvu Shooting 
Mtibwa Sugar 3 – 1 Ndanda FC 
Mbeya City 1 – 0 Coast Union 
Mgambo Shooting 0 – 1 Stendi United

No comments:

Post a Comment